Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, September 17, 2012

MIRAMBO NA MUHIMBILI ZATOKA SARE 2-2

Beki wa timu ya Muhimbili akiondosha mpira eneo la hatari wakati wa mchezo wa kirafiki na Mirambo jana jioni


Mchezaji wa Mirambo (mwenye jezi ya blue) akikimbia na mpira wakati wa mchezo wa kirafiki walioceza na Muhimbili kwenye uwanja wa Muhimbili jana jioni
TIMU za Veteran za Muhimbili na Mirambo zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana bao 2-2 kwenye mchezo uliochezwa juzi jioni kwenye uwanja wa Muhimbili.

Mchezo huo ulikuwa wa kuvutia sana kwani wachezaji hao wa zamami waliocheza ligi kuu walionyesha mbwembwe zao kwa pasi za kuonana na si kukimbia na mpira kama mtu anayefukuzwa.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyokuwa imeliona lango la mpinzani kutokana na umahiri wa beki kuwa makini.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko na Muhimbili ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la mashujaa wa Tabora Mirambo waishio hapa Dar es salaam kupitia kwa Clement Kahabuka.

Baada ya kufungwa bao hilo Mirambo walizinduka na ndipo Idd Moshi akasawazisha bao kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa Muhimbili.

Bao lingine la Mirambo lilifungwa na Wakulichombe Salum kwa shuti baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Muhimbili. Beki ya Mirambo ilijitahidi kulinda goli lakini ilijikuta Muhimbili wakisawazisha bao kupitia kwa Akida Makunda na kufanya matokeo yawe 2-2 hadi mwisho wa mchezo.

Wachezaji wa Mirambo walijikuta wanamlalamikia mwamuzi wakidai bao alilofunga Makunda mpira ulikuwa umetoka nje na kufanya mchezo kusimama takribani dk 3 kabla ya kuendelea tena.

No comments:

Post a Comment