U-17 wakienyeshwa jana na kocha wao Jacob Michelsen |
Hawa Kenya wamenikata stimu sana, wangekuja ningewakimbiza kama ninavyokukimbiza wewe. |
"Tunahakiki majina" je ni kweli ndio wewe |
Tumemaliza mazoezi tukutane kesho asubuhi |
Timu ya Taifa ya vijana Tanzania U-17 (Serengeti Boys) sasa itaivaa Misri kwenye raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 10 za Afrika kwa vijana zitakazofanyika mwakani nchini Morocco baada ya Kenya kujitoa.
Akizungumza na Habari za michezo, Afisa habari wa TFF Boniface Wambura alisema awali Serengeti Boys ilikuwa icheze raundi ya kwanza dhidi ya Kenya, Septemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) juzi lilituma taarifa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) likielezea kujitoa kwenye michuano hiyo.
Serengeti Boys itaanzia nyumbani Oktoba 14 mwaka huu, na marudiano itachezwa nchini Misri kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu. Mshindi baada ya mechi hizo mbili ataingia raundi ya tatu ambayo ndiyo ya mwisho kabla ya kwenda Morocco.
Katika raundi ya tatu ambayo mechi zake zitachezwa katikati ya Novemba na ya marudiano mwisho mwa mwezi huo, mshindi kati ya Tanzania/Misri atacheza na mshindi wa mechi ya Congo Brazzaville dhidi ya Msumbiji/Zimbabwe ambazo zinapambana katika raundi ya kwanza.
Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boys chini ya Kocha Jakob Michelsen ni makipa Abdallah Bakar, Hamad Juma na Peter Manyika.
Mabeki ni Abdallah Salum, Basil Seif, Hassan Mganga, Ismail Gambo, Mgaya Abdul, Miraji Selemani, Miza Abdallah, Mohamed Hussein, Pascal Matagi na Paul James.
Viungo ni Farid Musa, Hussein Twaha , James Mganda, Mbwana Ilyasa, Mohamed Haroub, Mohamed Kapeta , Mudathiri Yahya, Mzamiru Said na Selemani Bofu.
Washambuliaji ni Abdallah Kisimba, Calvin Manyika, Dickson Ambunda, Joseph Lubasha, Kelvin Friday na Salvatory Nkulula
No comments:
Post a Comment