KAMATI YA SHERIA KUPITIA USAJILI SEPT 2
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya
Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka
huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2012/2013.
Usajili utakaopitiwa ni wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na
Lidi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo Kamati itapitia pingamizi zilizowasilishwa
na klabu mbalimbali dhidi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu zingine.
No comments:
Post a Comment