Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 29, 2012

Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB) kimetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Robert Makanja ili aweze kucheza mpira wa miguu nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema DFB imetuma maombi  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya TUS Ahausen, Hessischer FuBall-Verband ambayo hata hivyo haikuelezwa iko ligi ya daraja gani nchini humo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mashindano wa DFB, Markus Stenger, Mtanzania huyo ameombewa hati hiyo kama mchezaji wa ridhaa kwa maelezo kuwa hakuwahi kusajiliwa na klabu yoyote nchini.

TFF inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika kukamilika ikiwemo kubaini kama kweli mchezaji huyo hakuwahi kusajili na klabu yoyote hapa nchini.
**********************************************************************************


TIMU ya soka ya wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Mahakama kesho kwenye uwanja wa shule ya msingi Muhimbili jijini Dar es salaam.

Akizungumza na BINGWA kocha msaidizi wa mambo ya nje Japhet Chaula alisema mchezo utaanza majira ya saa kumi jioni ili kwasababu ijumaa ni siku ya kazi.

Pia mchezo huu utakuwa mahususi kwa timu yetu ili wapate nafasi ya kufanya marekebisho kwa nafasi ambazo zitaonekana zina mapungufu.

"Mahakama ni timu nzuri ndio maana tumeomba tucheze mchezo nao ili kujipima uwezo na kama kutaonekana nafasi zenye mapungufu zifanyiwe marekebisho mapema" alisema Chaula.


Timu hizi zinatumia mchezo huu katika kujipima nguvu kwani zipo kwenye maandalizi ya mashindano ya SHIMIWI kwa wanategemea mwaka huu kutakuwepo na ushindani mkubwa sana.

SHIMIWI ni shirikisho la michezo ya wizara na taasisi za umma ambayo yanatarajiwa kutimua vumbi mkoani Morogoro kuanzia Septemba 22 hadi Octoba 5 mwaka huu.
***************************************


UONGOZI wa chama cha soka manispaa ya Mbeya (MUFA) unavitangazia timu zinazotaka kushriki ligi daraja la nne kuwa mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni leo kwenye ofisi zao zilizopo uwanja wa Sokoine mkoani hapo.

Akizungumza kwa njia ya simu na BINGWA mwenyekiti wa MUFA, Seleman Haroub alisema kuwa mwisho wa kuchukua fomu kwa vilabu ni Agosti 30 baada ya hapo kamati itakaa kupitia maombi yote ya vilabu

Pia alivitaka vilabu zijaze fomu za usajili vizuri na kufanya uhamisho kwa wachezaji kwa kufuata taratibu ili kukwepa kukatiwa rufaa au kuwekewa pingamizi.

"Napenda kuvitangazia vilabu kuwa mwisho wa kuchukua fomu za kuomba kushiriki ligi daraja la nne ni agosti 30 baada ya hapo kamati itakaa kupitia maombi yote na pia uongozi wa vilabu ufuate taratibu katika kuhamisha na kusajili wachezaji ili kuepuka kuwekeana pingamizi au kukatiwa rufaa" alisema Seleman.

Ligi daraja la nne inaanza kuchezwa nchini kote mwaka huu baada ya shirikisho la soka nchini kutangaza kuirudisha mapema Agosti mwaka huu kwani ilifutwa takribani miaka sita.

TFF ilifuata ligi ya madaraja lakini imeirudisha tena baada ya kuona kuwa timu ambazo wachezaji hawachezi mechi nyingi na vilabu vyenye uwezo kifedha ndivyo vilikuwa vinafaida na mfumo huo

No comments:

Post a Comment