MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI
SEPT 27
Shirikisho la Mpira wa miguu
Tanzania limeandaa mtihani kwa ajili ya
watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Septemba 27 mwaka huu saa 4
kamili asubuhi ofisi za Shirikisho
Kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa
kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze
kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya
kwanza ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF. Ada ya mtihani ni
dola 50 za Marekani.
Pia Damas Ndumbaro na Ally Mleh wa
Manyara Sports Management ambao tayari ni mawakala wanaotambuliwa na FIFA
wanatakiwa kufanya mtihani huo kama wanataka kuendelea na uwakala kwa vile muda
wa leseni zao za awali umemalizika.
Mawakala wengine ambao ni John
Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully leseni zao
bado ziko hai.
No comments:
Post a Comment