Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, August 31, 2012

Serengeti boys waliopo kambini

SERENGETI KUJIPIMA NA ASHANTI
TIMU ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyopo kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya itavunja rasmi kambi yake leo kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ashanti United.

Serengeti boys na  Ashanti United iliyoko daraja la kwanza itacheza kuanzia saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh. 2,000 tu.

Timu hii ya vijana ilikuwa Septemba 9 mwaka huu icheze na Kenya kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, lakini Kenya ikajitoa ambapo sasa itacheza na Misri katika raundi ya pili. Mechi ya kwanza itachezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwishoni mwa Septemba, Serengeti Boys itarejea tena kambini kujiandaa kuikabili Misri ambapo kabla inatarajia kupata mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu itakayotangazwa baadaye.

Naye kocha wa Ashanti United Mubaraka Mohamed amesema amefurahi kupata nafasi ya kucheza na Serengeti boys kwani ni wachezaji wazuri na atapata nafasi ya kukipima kikosi chake kabla ya ligi daraja la kwanza kuanza.

"Serengeti boys ni timu bora kwani inaundwa na wachezaji wenye vipaji hivyo naamini ni fursa ya mimi kocha kukiangalia na kupima kikosi kabla ligi ya daraja la kwanza haijaanza", alisema Mubaraka.

No comments:

Post a Comment