SERENGETI BOYS, KUCHEZA NA KENYA AZAM COMPLEX
Mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za 10 za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwakani
nchini Morocco kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Kenya itachezwa Septemba 9
mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Tayari Serengeti Boys chini ya Kocha Jakob Michelsen na Msaidizi
wake Jamhuri Kihwelo ikiwa na wachezaji 28 iko kambini jijini Dar es Salaam
tangu jana (Agosti 27 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10
kamili jioni.
Wachezaji waliko kambini ni makipa Abdallah Bakar (Mjini
Magharibi), Hamad Juma (Azam) na Peter Manyika (JKT Ruvu). Mabeki ni Abdallah
Salum (Mjini Magharibi), Basil Seif (Morogoro), Hassan Mganga (Morogoro),
Ismail Gambo (Azam), Mgaya Abdul (Azam), Miraji Selemani (Polisi Morogoro),
Miza Abdallah (Kinondoni), Mohamed Hussein (Azam), Pascal Matagi (Dodoma) na
Paul James (Kinondoni).
Viungo ni Farid Musa (Kilimanjaro), Hussein Twaha (Coastal Union),
James Mganda (Kipingu Academy), Mbwana Ilyasa (Simba), Mohamed Haroub
(Zanzibar), Mohamed Kapeta (Kinondoni), Mudathiri Yahya (Azam), Mzamiru Said
(Morogoro) na Selemani Bofu (JKT Ruvu).
Washambuliaji ni Abdallah Kisimba (Mwanza), Calvin Manyika
(Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza), Joseph Lubasha (Azam), Kelvin Friday (Azam)
na Salvatory Nkulula (Kipindu Academy).
Mechi ya marudiano itachezwa jijini Nairobi, Kenya kati ya
Septemba 21, 22 na 23 mwaka huu. Timu itakayofanikiwa kusonga mbele itacheza
raundi ya pili dhidi ya Misri. Mechi ya kwanza itachezwa nyumbani kati ya
Oktoba 12, 13 na 14 mwaka huu wakati ya marudiano itakuwa kati ya Oktoba 26, 27
na 28 mwaka huu.
Misri ni kati ya timu 17 zilizoingia moja kwa moja raundi ya pili.
Nyingine ni Afrika Kusini, Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Congo Brazzaville,
Cote d’Ivoire, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Mali, Rwanda, Senegal, Sierra
Leone, Tunisia na Zambia.
No comments:
Post a Comment