WAZIRI SANGU AMPOKEA WAZIRI WA KAZI WA QATAR, TAYARI KWA DOHA DIALOGUE II

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu, amempokea Waziri wa Kazi wa Qatar, Mhe. Dkt. Ali bin Samikh Al Marri, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2026 kwa lengo la kushiriki Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue.

Katika mapokezi hayo, Waziri Sangu ameambatana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Evaline Munisi.

Aidha, Ujio wa Waziri wa Kazi wa Qatar nchini ni kiashiria cha kuanza kwa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue, unaotarajiwa kuwakutanisha wawakilishi kutoka nchi za Umoja wa Afrika (AU) pamoja na nchi za Ghuba (GCC+).



Mkutano huo unalenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika na nchi za Ghuba katika kuhakikisha kunakuwa na uhamaji wa nguvu kazi wenye haki na endelevu. Mkutano huo utafanyika tarehe 5 - 6 Oktoba, 2026 ukiongozwa na kaulimbiu isemayo: “Kutoka Ahadi hadi Vitendo: Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu Kazi wenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+).”

No comments