MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MAZIKO YA HAFIDH AMEIR HASSAN- MWENZA WA RAIS

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki maziko ya marehemu Hafidh Ameir Hassan, ambaye ni mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, ltarehe 07 Septemba 2026.

Maziko hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Viongozi Wakuu Wastaafu, Viongozi wa Serikali, Dini, Vyama vya siasa, Viongozi wa Mahakama, Bunge, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, familia, marafiki pamoja na waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Marehemu Hafidh Ameir Hassan amefariki  tarehe 07 Septemba 2026 katika Hospitali ya kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.









No comments