SALAMU ZA RAIS TSHISEKEDI WA DRC KWA RAIS SAMIA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 19 Julai, 2026, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mheshimiwa Félix Antoine Tshisekedi.

Ujumbe huo umewasilishwa rasmi na Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa DRC, Mhe. Floribert Anzuluni Isiloketshi, katika Ikulu jijini Dar es Salaam. 



Katika mazungumzo yaliyofanyika wakati wa makabidhiano hayo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Mhe. Isiloketshi kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu pamoja na undugu uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa nchi zote mbili.

No comments