Billnass na Nandy waadhimisha miaka minne ya ndoa kwa mbwembwe



Mastaa wa Bongo fleva, William Lyimo ‘Billnass’ na Faustina Charles ‘Nandy’ wameadhimisha kumbukumbu ya miaka minne ya ndoa yao kwa sherehe ya kifahari iliyofanyika nyumbani kwao Goba, Dar es Salaam, ikiwa ni miaka tangu walipofunga ndoa Julai 16, 2022 na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Naya. 

Katika maadhimisho hayo yaliyozua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii, Nandy alipokea zawadi maalumu ya cheni ya Tiffany kutoka kwa mumewe Billnass, huku wakitania na kusherehekea kwa staili ya kipekee ambapo Billnass alijifananisha na ‘muuza madini wa Katoro’ kwa kumwagia zawadi na kumpa heshima mke wake.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Nandy alimshukuru mumewe kwa kumheshimu kama mke, wakati Billnass alieleza kuwa Nandy ana sifa zote alizokuwa akimuomba Mungu azipate kwa mwanamke wa maisha yake, huku wanandoa hao wakizidi kuonesha ukaribu na kusherehekea mafanikio na safari yao ya upendo tangu wafunge ndoa.


No comments