SERIKALI YAJIVUNIA UIMARA WA UCHUMI
Serikali imepata
mafanikio makubwa katika kusimamia uchumi wa nchi ambapo Pato la Taifa
limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 5.1 mwaka 2024, huku mfumuko wa bei
ukidhibitiwa kubaki ndani ya lengo la asilimia 3.0 hadi 5.0, hali inayotoa
ahueni kwa maisha ya Watanzania.
Mafanikio haya
yameenda sanjari na hatua ya kihistoria ya kuzindua mchakato wa Dira ya Taifa
ya Maendeleo 2050 ambayo sasa inatoa mwelekeo mpya wa nchi kuelekea uchumi wa
kipato cha juu ifikapo nusu ya karne. OUA
YA BAJETI YA OFI YA
Hayo yamesemwa
na Profesa Kitila Mkumbo wakati akisoma
Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Bungeni leo.
Prof Kitila pia
alisema kwamba Serikali katika kuimarisha uwekezaji, imefanikiwa kusajili
miradi ya uwekezaji yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.48 kupitia
Kituo cha Uwekezaji (TIC), hatua iliyochochewa na maboresho ya sera na sheria
yaliyofanywa kwa makusudi ili kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara na uzalishaji
katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Sambamba
na mafanikio hayo, usimamizi wa Mashirika ya Umma umeshuhudia mageuzi makubwa
ambapo Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanikiwa kukusanya mapato yasiyo ya kodi
ya kiasi cha shilingi bilioni 773.37 hadi kufikia Machi 2026, ikiwa ni ongezeko
la asilimia 16 ndani ya mwaka mmoja.
Aidha Serikali
imefanikiwa pia kukamilisha mapitio ya mfumo wa kisheria wa uwekezaji wa umma
na kuunganisha baadhi ya taasisi ili kuongeza tija na kupunguza mzigo wa
gharama za uendeshaji kwa mlipa kodi.
Aidha, kuanzishwa
kwa Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZ) kumeleta matokeo chanya kwa kusajili miradi
inayotoa ajira kwa vijana na kukuza mauzo ya bidhaa nje ya nchi, jambo ambalo
limeimarisha akiba ya fedha za kigeni na kuifanya nchi kuwa na ustahimilivu wa
kiuchumi licha ya changamoto za kijiopolitika duniani.

Post a Comment