WABUNGE VITI MAALUMU HAWA HAPA

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele (katikati) akiongoza kikao cha Tume kilichokutana Jijini Dodoma leo Novemba 7, 2025 na kupitisha majina ya wabunge wa viti maalum. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume , Mhe. Jaji wa Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk na kushoto ni Katibu wa Tume ambae pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima. (Picha na INEC). 

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza majina 115 ya wabunge wanawake wa viti maalumu kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa uchaguzi wa INEC Ramadhan Kailima, CCM imepata viti 113 na CHAUMMA viti viwili. Kailima alisema katika taarifa hiyo kuwa idadi ya wabunge hao inapawa kuwa 116 lakini nafasi ya mbunge mmoja uteuzi wake utafanyika baada ya kukamilika uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Fuoni Zanzibar na jimbo la Siha Tanzania Bara.

Majimbo hayo hayakufanya uchaguzi wa wabunge baada ya kufariki kwa wagombea kukiwa kwenye mchakato wa uchaguzi.

Idadi ya wabunge wa viti maalumu hutokana na wingi wa kura inazopata chama kwenye nafasi ya urais, kwa uchaguzi wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 29, mgombea wa CCM Samia Suluhu Hassan alishinda kwa kura 31,913,866 huku mgombea wa CHAUMMA Salum Mwalimu akipata kura 213,414. 

Katika taarifa ya Kailima, miongoni mwa majina ya wabunge waliochomoza kwenye nafasi hizo ni aliyekuwa mbunge wa jimbo la Segerea Bona Kamoli, Mkurugenzi wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’’ Asha Baraka na Khadija Shabani (Keisha) ambaye awamu iliyopita aliwakilisha watu wenye ulemavu.

Wengine walioteuliwa ni Agness Hokororo, Agness Marwa, Aisha Mduyah, Amina Mzee, Amina Said, Amina Mabrouk, Asha Feruzi, Asha Rashid, Asha Motto, Asya Khamis, Asya Omar, Athumini Mapalilo,Aysharose  Mattembe, Aziza  Ally, Catherine Joachim, Cecilia Paresso, Chiku Issa, Christina Mnzava, Christina Mndeme,  Devotha Mburarugaba, Esther  Midimu, Esther Malleko, Fatma Rembo, Ghati  Chomete, Grace Mkoma, Halima Bulembo, Halima  Nassor na Happiness Ngwado.

Hawa Chakoma, Husna Sekiboko, Jacqueline Mzindakaya, Jacqueline Andrew, Jacqueline Ngonyani (Msongozi), Jamila Juma, Janeth Mahawanga, Janeth Pinda, Jasmine Ng’umbi, Jesca Magufuli, Jesca Mgogo, Josephine Kapoma, Josephine Chagula, Juliana Shonza, Kabula Shitobela, Khadija Aboud, Kijakazi Yunus, Latifa Juwakali, Lucky Mwakyembe, Lucky Kombani, Lulu Mwacha, Magreth Ezekiel, Mariam Ibrahim, Mariam Mungula, Mariam Nyoka, Mariam Ussi Yahya, Marirta Kivunge, Martha Mariki, Martha Gwau.

Wengine ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mary Chatanda, Mary Masanja, Maryam Mwinyi, Maryprisca Mahundi, Mgeni Hassan Juma, Mvita Mustafa Ali, Mwanaenzi Hassan Suluhu, Mwanahamisi Athumani Munkunda, Mwanaisha Ulenge, Mwantatu Mbarak Khamis, Mwantumu Zodo, Nadra Gulam Rashid, Najma Murtaza Giga, Nancy Nyalusi, Maomy Mwaipopo, Nasriya Nassir Ali,   Neema Mwandabila, Neema Majule, Neema Mgaya, Ng’wasi Kamani, Nyamizi Mhoja, Pindi Chana, Rahma Kisuo, Rebeca Nsemwa, Regina Malima, Regina Mikenze, Regina Qwaray, rose Tweve, Salome Makamba, Samira Amour, Santiel Kirumba, Selina Kingalame.

Pia wamo Shadya Haji Omar, Sheila Lukuba, Sikudhani Chikambo, Stella Alex, Suma Fyandomo, Sylivia Sigula, Tamima Haji Abass, Taska Mbogo, Tauhida Gallos, Timida Fyandomo, Tinnar Chenge, Tunu Kondo, Ummy Nderiananga, Yumna Omar, Yustina Rahhi, Zainab Katimba, Zainab Abdallah Issa, Zainab Kawawa, Zena Maulidi Katambo, Zeyana Abdallah Hamid, Zuena Athumani Bushiri.

Kwa upande wa CHAUMMA, wabunge walioteuliwa ni aliyekuwa mgombea mwenza Devotha Minja na Sigrada Mligo.

Mwisho.

No comments