DAR INAPOJIANDAA KUWA ‘MEGA CITY’: KURA YAKO NI MUHIMU
Na Mwandishi Wetu
Kila mara
tunapokaribia uchaguzi, mijadala hujawa na mbwembwe, matusi na maneno matupu
yanayopoteza muda. Lakini Uongozi wa kweli sio makelele jukwaani; ni uwezo wa kutafsiri
maono makubwa kuwa matendo halisi yanayoleta maendeleo na fursa za ajira
kwa wananchi.
Huu ndio wakati
wa kuingia kwenye sanduku la kura kuamua mabadiliko kwa kutambua kiongozi anayesema
ukweli unaogusa mahitaji yetu ya msingi na anayeweza kusimamia mabadiliko
yaliyokusudiwa.
Kiukweli, kura
yako ni muhimu sana kwani inatoa mamlaka ya kusimamia mabadiliko makubwa ya
Taifa hili. Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania inaendelea kuandika
historia mpya ya maendeleo kupitia miradi mikubwa ya usafiri wa kisasa na
kazi hii inahitaji usimamizi wa karibu.
Baada ya
mafanikio makubwa ya Reli ya Kisasa (SGR) inayotumia umeme, sasa macho
ya Watanzania yanaelekezwa kwenye hatua nyingine kubwa zaidi ya kuboresha
miundombinu ya usafiri.
Mtaalamu wa
Miundombinu, Bw Salum Mturi, anasisitiza: "Kama hatutapiga kura kwa kiongozi
mwenye maono ya miundombinu, tutabaki kwenye foleni kwa miaka mingine mitano.
Kura yetu ndiyo inahakikisha Serikali inaendelea na kasi hii."
Chini ya uongozi
wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mpango uko tayari wa kuanza ujenzi wa treni
za mijini (Metro) katika majiji ya Dar es Salaam na Dodoma katika
kipindi cha miaka mitano ijayo. Mradi huu ni sehemu ya mpango mpana wa
kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza msongamano, kurahisisha
usafiri, na muhimu zaidi, kukuza uchumi wa mijini.
Wakati Dar es
Salaam inajiandaa kuwa “megacity” ya kwanza Afrika Mashariki yenye wakazi zaidi
ya milioni 10,
Mradi wa Metro na ujenzi wa miundombinu inayouzunguka unahakikisha ukuaji huu
wa watu unakwenda sambamba na ufanisi wa usafiri. Huu si tu ujenzi wa
miundombinu; ni injini ya kutoa ajira kulingana na mahitaji yetu halisi.
Maeneo kama Morocco,
Mwenge, Magomeni na Tabata yanatarajiwa kupata barabara za juu
(flyovers), ambayo yanatarajiwa kujengwa barabara hizo yanamaanisha kazi
nyingi za ujenzi, uhandisi, na usimamizi.
Bi. Neema
John, mhitimu wa Uhandisi (25), anasema: "Miradi mikubwa kama flyovers
na Metro inamaanisha ajira kwetu. Mimi sitapiga kura kwa maneno matupu,
nitapiga kura kwa yule anayeonesha wazi mahali pa kwenda kufanya kazi."
Kila mradi
unaotekelezwa, ukiwemo wa Arena (ukumbi mpya wa kimataifa utakaobeba
watu 15,000) katika eneo la Kawe, unatafsiriwa kuwa fursa mpya za ajira
ndogondogo na uwekezaji katika sekta binafsi.
Kama ilivyokuwa
ndoto kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa saa moja kupitia SGR,
sasa treni za Metro zitakuwa ishara ya zama mpya za ufanisi na teknolojia. Huu
ndio ukweli tunaokubaliana nao kama mahitaji yetu.
Acha Mbwembwe
Wakati wa kupiga
kura, acha kupoteza muda na mbwembwe na badala yake, angalia matokeo
ya kazi. Kura yako lazima iwe kwa dira ya maendeleo, kasi, na uthubutu
ambayo inajibu moja kwa moja mahitaji ya ajira na maisha bora ya mwananchi.

Post a Comment