Athena yaajiri mbobezi kusukuma mbele ujenzi miundombinu ya kidjiti Afrika Mashariki
Na Mwandishi wetu
Athena Core Technologies, kampuni inayojenga miundombinu ya kidijitali Afrika Mashariki,
imetangaza kumteua Jorge Rodriguez
kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wake mpya.
Rodriguez, ameshashika nyadhifa za utendaji katika kampuni
ya América Móvil (pamoja na Telmex USA, Claro Enterprise Solutions, na HITSS
USA) na hivi karibuni Sorenson Communications.
Uteuzi wa Rodriguez umefanyika wakati Athena ikipanua shughuli
zake kwa kuhakikisha uwapo wa jukwaa jumuishi la kidijitali litakalohusisha nyaya za chini ya bahari (subsea capacity),
vituo vya data visivyo na upendeleo
(carrier-neutral data centers), na mkongo wa kitaifa (nationwide fiber networks).
Ujenzi wa miundombinu hiyo imekusudiwa kutoa njia mbadala
za mawasiliano yenye kasi na ufikiaji wa uhakika wa intaneti katika ukanda wote
wa Afrika Mashariki.
Rodriguez mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika uongozi wa sekta za
mawasiliano na teknolojia duniani, akikuza majukwaa makubwa ya mawasiliano
katika nchi za Amerika na maeneo mengine, huku akionesha rekodi nzuri ya kuleta
mabadiliko chanya ya kiutendaji amesisitiza umuhimu wa jukumu la Athena katika
kuunganisha mataifa, kuwezesha ukuaji wa uchumi, na kuunda Afrika inayoongozwa
na kipaumbele cha teknolojia ya 'cloud'.
Uzoefu na dira ya Rodriguez unatazamiwa kuimarisha nafasi
ya Athena kama kinara wa soko katika kutoa miundombinu ya kidijitali
inayoaminika na yenye ufanisi barani.
Athena Core Technologies imelenga kuziba pengo la
kidijitali na kuwawezesha serikali, biashara, na jamii kustawi .
Post a Comment