KARIA : Tumetengeneza Kanuni na Bodi watakuwa wanazisimamia

 



Na Rahel Pallangyo,  Tanga

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amesema shirikisho litabaki kutunga kanuni  na Bodi ya Ligi itabaki kuwa wasimamizi wa kanuni hizo.


Karia alisema hayo jijini  Tanga baada ya kuthibitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu kuendelea kuongoza TFF kwa kipindi kingine cha miaka minne.


"Nawashukuru wadau wote jambo letu limekwisha salama, niwahakikishie Watanzania kuwa nitaendelea kusimamia mpira wa miguu.


 Tutashirikiana na wadau wote wala hakuna mtu mwenye dhamira ya kulipa kisasi kwa sababu hayo yote yaliuofanyika ni michakato ambayo Mungu amepanga wapite katika misukosuko ili wawe bora zaidi.


"Haikuwa rahisi kwa mchakato huu wa uchaguzi na wajumbe msiumie kwa nyakati ngumu zilizotokea hivi karibuni kwani hatua hiyo imekuwa ni sawa na kupitisha chuma kwenye moto ili kiwe imara.


"Misukosuko tuliyopitia ni ishara kwamba tunachangamoto kwa hiyo tunatakiwa kwenda kuzifanyia kazi ma nawashukuru kwa imani yenu kwangu na wenzangu, kitu tunachotakiwa kufanya sasa ni kila mmoja akafanye kazi yake, tutakwenda kuendelea kusimamia uendeshaji mzuri wa mpira wetu," alisema Karia.


Alisema ile kutaja TFF/Bodi ya Ligi wameiondoa kwenye kanuni na kubaki Bodi ya Ligi kwa sababu kelele nyingi zimetoka kwenye masuala ya uwezeshaji wa Bodi ya Ligi.

"Ile kutaja TFF/Bodi ya Ligi tumeiondoa kwenye document zote na mpaka kwenye kanuni tumeondoa, sisi tutabaki kutengeneza kanuni na wao watakuwa wanazisimamia maana kelele nyingi zimetoka kwenye masuala yale yauwezeshaji wa Bodi ya Ligi hivyo masuala ya bodi Karia hausiki tena tusitiane vidole vya macho bure" alisema.


Alisema shirikisho lina mambo mengi ya kusimamia ya maendeleo ya mpira wa miguu kwani hata kituo cha Mnyanjani Tanga kimekuwa FIFA talent academy.

No comments