ya Taifa ya Tanzania Bara U20 imeibuka bingwa wa mashindano
ya CECAFA baada ya kuifunga timu ya Kenya kwa bao 1-0 katika mchezo uliochwezwa
kwenye Uwanja wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA Technical Centre) uliopo
Njeru, Jinga na Eritrea ikishika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Sudan 1-0
Katika
mchezo huo ambao ulijaa ufundi Tanzania Bara ilipata bao katika dakika za
nyongeza za kipindi cha kwanza baada ya mchezaji wa Kenya John Ochieng
kujifunga na kuifanya kwenda mapumziko ikiwa mbele.
Baada
ya kutoka mapumziko Kenya walifanya mabadiliko ya kumtoa Ronald Sichenje na
kuingia Benson Ochieng dakika ya 50 na dakika ya 65 Tanzania Bara
ilimtoa mshambuliaji Luyaya Said na kuingia Andrew Albart na kufanya kila timu
kuongeza mashambulizi.
Akizungumza
baada ya mchezo Kocha Zuberi Katwila alisema waliingia kwenye mchezo wakijua
wanakwenda kushinda kwa sababu walishawasoma Kenya wanavyocheza.
“Namshukuru
Mungu kwa sisi kuwa mabingwa lakini tuliingia kwenye mchezo tukijua tunakwenda
kushinda kwa sababu tulishaisoma Kenya jinsi wanavyocheza kwani hata hatua ya
makundi tulitoka nao sare ya mabao 2-2,” alisema Katwila
Katika
mashindano hayo Kelvin John wa Tanzania Bara aliibuka mfungaji bora akiwa na
mabao saba akifuatiwa na mshambuliaji mwenzake Andrew Simchimba ambaye alifunga
mabao sita sawa na Yoseif Tesfai wa
Eritrea.
Tanzania Bara ilifuzu fainali baada ya kuifunga Sudan kwa mabao 2-1 na Kenya ikaifunga Eritrea kwa bao 1-0.
Mpaka
kutinga fainali Tanzania Bara ilifunga mabao 17 na imefunga mabao matano tu,
mawili katika hatua ya makundi, mawili robo fainali na moja nusu fainali.
Mashindano
ya CECAFA U20 yalianza kutimua vumbi Agosti 22, Tanzania bara ikiwa katika
Kundi B pamoja na timu za Ethiopia, Zanzibar na Kenya na kundi A lilikuwa na
timu za Uganda, Sudan, Sudan Kusini na Eritrea.
No comments:
Post a Comment