WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza benki
ya Standard Chartered kwa kutumia ufadhili wao kwa timu ya Liverpool kuboresha
soka hapa Tanzania.
Akizungumza
kwa niaba ya Dkt. Mwakyembe, wakati wa fainali za kuwania kombe la The Standard Chartered Cup 2019 kwenye
viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24,
2019, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodgar Tenga alisema,
“Nimekuwa
nikifuatilia kwa karibu sana jinsi benki hii imekuwa ikileta magwiji wa timu ya
Liverpool hapa nchini ambapo mwaka juzi 2017 walimleta John Barnes na mwaka
jana 2018 alikuja Sami Hyypia ambao kwa nyakati walizokuja walikuwa na
ratiba hapa nchini iliyohusisha mafunzo ya soka kwa makundi mbalimbali ya
watoto na timu za vijana wetu kama vile Serengeti Boys kwetu sisi hili ni jambo
la kupongezwa.” Alisema Tenga akimnukuu Dkt. Mwakyembe.
Awali
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard
Chartered Bank, Ajmair Riaz alisema hii ni mara ya Nne kwa benki yake kuandaa
mashindano hayo ambapo mwaka huu zaidi ya timu 25 zilishiriki huku timu
inayotwaa kombe pia hupata nafasi ya kwenda nchini Uingereza kushuhudia live pambano la soka baina ya Liverpool
na Watford litakalopigwa Desemba mwaka huu 2019 kwenye uwanja wa Andield.
Naye
Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Walles Karia alisema, Shirikisho hilo
litatoa kila aina ya ushirikiano kwa taasisi yoyote ile ikiwemo benki ya Standard Chartered katika kukuza soka
hapa nchini.
Katika
hafla hiyo, pia Balozi mdogo wa Uingereza nchini, Rick Shearn alipata fursa ya
kutoa salamu za ubalozi huo kwa washiriki wa fainali hizo kwa kusema, “Mpira ni zaidi ya michezo huleta pamoja
jamii, lakini pia mpira hufundisha utulivu, ubunifu na nidhamu ambavyo
ni somo linaloweza kutumika katika maisha yetu ya kila siku.” Alisema Kaimu
balozi huyo hapa nchini.
Timu ya Dar es Salaam Corridor ndiyo iliyoibuka mshindi katika fainalki hizo kwa kuichapa timu ya Coca Cola kwa bao 1-0 na hivyo ndiyo itakayokwenda nchini Uingereza Desemba mwaka huu 2019 kushuhudia Live pambano la soka ligi kuu ya Uingereza kati ya Mabingwa Liverpool na Watford kwenye uwanja wa Anfield.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodgar Tenga (kulia), akizunguzma jambo na Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz (kushoto) na Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Wallace Karia (wapili kushoto) na Balozi Mdogo wa Uingereza Nchini, Rick Shearn muda mfupi kabla ya kuanza kwa fainali hizo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard
Chartered Bank, Ajmair Riaz akipoiga mpira kuashiria kuanza kwa fainali hizo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodgar Tenga (aliuesimama), akitoa hotuba yake ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Habari, Uramaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, muda mfuoi kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019.
Timu ya Coca Cola na Airtel zikichuana kwenye pambanpo la awali la fainali hizo.Coca Cola ilishinda mabao 2-0.
Mchezaji wa Halotel (katikati) akiwa kwenye msukosuko kutoka wapinzani wake
Mchezaji wa Sahara Midia Group akimenyana na mchezaji wa Pasada (aliyevaa jezi za blue)
Mchezji wa IPP (aliyevaa kifani) na mchezaji wa Wanasheria wa East Africa Lawa Chamber, wakimenyana kuwania mpira.
Balozi mdogo wa Uingereza nchini, Rick Shearn (kulia), akibadilishana mawazo na Mchezaji wa soika wa zamani na mchambuzi wa mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini, Ally Mayayi Tembele.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank, Ajmair Riaz (kulia) na Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki hiyo, Juanita Mramba wakiwa eneo la tukio.
Rais wa TFF akiwa tayari amekabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Dar es Salaam Corridor (watatu kulia) huku akisaidia kulibeba na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Charteredb Bank Ajmi Riaz
No comments:
Post a Comment