Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, September 4, 2019

ZAHERA AFUNGIWA MECHI TATU NA MASAU ATOZWA FAINI YA 200,000

Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Septemba 2, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020 iliyoanza rasmi Agosti 24, 2019 na kufanya uamuzi ufuatao;
Mechi namba 9- Yanga 0 vs Ruvu Shooting 1. Mwamuzi Msaidizi Janeth Balama amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kutafsiri sheria, hivyo kusababisha akatae bao halali lililofungwa na Ruvu Shooting katika mechi hiyo iliyofanyika Agosti 28, 2019 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi hiyo, kinyume na Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
Klabu ya Yanga imepewa Onyo Kali kwa kushindwa kuhakikisha Kocha wake Mwinyi Zahera anaongoza benchi la ufundi la timu yake akiwa katika mavazi nadhifu na ya heshima. Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mkurugenzi wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametozwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili), kwa kuingia ndani ya uwanja (eneo la kuchezea) baada ya filimbi ya mwisho, kinyume na Kanuni ya 14(10) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungiwa kuiongoza timu yake katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kutoa shutuma na kejeli kwa Bodi ya Ligi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

No comments:

Post a Comment