MABINGWA
watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameendelea kupeleka presha kwa Simba baada
ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo
uliochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Yanga imerejea katika nafasi ya pili na
kuendelea kumfukuza mnyama kimya kimya kwa kufikisha pointi 43 ikizidiwa pointi
tatu na Simba huku kila timu ikiwa imeshuka dimbani mara 20.
Hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika, timu hizo zilikuwa suluhu na kuwafanya mashabiki wa Yanga kuwa na
hofu wakihofia timu yao huenda ikalazimishwa sare.
Kipindi cha pili kilikuwa
na neema kwa Yanga, ambapo mnamo dakika ya 53, Ibrahim Ajib alifunga bao la
kwanza kwa njia ya penalti, baada ya beki wa Kagera Sugar kuunawa mpira
katika eneo la hatari.
Yanga iliendeleza makali
katika kipindi cha pili na katika dakika ya 77 ya mchezo huo, 77, Emmanue
Martin alifunga bao la pili baada ya
kupata pasi ya Chirwa na kufanya timu hiyo kuwa mbele kwa mabao 2-0.
Kazi nzuri ya Mhilu ilizidi
kuzaa matunda tena, ambapo katika dakika ya 88, Godfrey Taita alijifunga,
kufuatia kazi nzuri ya Mhilu aliyepiga shuti kali lilisababisha mchezaji huyo
wa Kagera kujifunga.
Yanga sasa ina pointi 43
ikiwa nafasi ya pili, huku Simba ina alama 46, na Azam imeshuka hadi nafasi ya
tatu ikiwa na alama zake 41.
Yanga imeibuka na ushindi
huo baada ya Jumanne kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Township Rollers
ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment