WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwa mujibu wa
Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho
yake ikisomwa na muundo wa shughuli za
Baraza, amemteua Leodger Chilla Tenga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la
Taifa.
Dk.
Mwakyembe amewateua pia wajumbe wapya sita wa Baraza hilo kama ifuatavyo:
1.
Profesa Mkumbwa
M. A. Mtambo.
2.
Beatrice Singano.
3.
Kanali
Mstaafu Juma Ikangaa.
4. John
Joseph Ndumbaro.
5. Rehema
Sefu Madenge.
6.
Salmin
Kaniki.
Aidha, Dk.
Mwakyembe amewateua wajumbe wengine watatu wa Baraza kutokana na nafasi za vyeo
vyao ambao ni:
1.
Yussuph
Singo - Mkurungezi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na
Michezo.
2.
Dk.
Edicome Shirima- Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.
3.
Mohammed
Kiganja-Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa ambaye atakuwa ni Katibu wa
Baraza.
Uteuzi wa
wajumbe wote umeanza rasmi Februari 8, 2018 na watalitumikia Baraza kwa kipindi
cha miaka mitatu
Vilevile
Dk. Mwakyembe kwa mujibu wa sheria amemteua Timothy Mganga kuwa Mkuu wa Chuo
cha Maendeleo ya Michezo Malya kwa kipindi cha miaka mitano.
No comments:
Post a Comment