MWAMUZI wa Kimataifa,
Hery Sasii anatarajiwa kuwa pilato wa mchezo wa Ligi Kuu Bara, raundi ya nane
utakaozikutanisha Yanga na Simba Oktoba 28 mwaka huu.
Sasii wa Dar es
Salaam ndiye aliyechezesha mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya watani hao
uliomalizika kwa Simba kushinda kwa mikwaju ya penalti 5-3.
Mwamuzi huyo
atasaidiwa na mwamuzi msaidizi wa kimataifa Soud Lila wa Dar es Salaam na
Mohamed Mkono wa Tanga na mezani atakuwepo mwamuzi msaidizi wa kimataifa,
Josephat Bulal.
Sasii nje ya uamuzi
ni fundi katika kampuni ya Itech Contractors, katika uwekaji wa vioo na kufanya
marekebisho (maintenance) katika majengo pia anamiliki duka la vifaa vya
ujenzi.
Akizungumza jana,
Sasii alisema amesomea ufundi wa umeme
wa majumbani na wa magari lakini pia alisomea kozi ya ufundi wa kupaua majengo
lakini hakuimaliza.
“Mimi nafanya
biashara ya mbao na ninamiliki kiwanda kidogo cha kuranda mbao na duka la vifaa
vya ujenzi lakini nafanya kazi katika kampuni ya Itech Contractors,” alisema
Sasii.
Sasii mwamuzi ambaye
anamudu vema kupiga filimbi, kusimamia sheria 17 za soka na asiyeyumbishwa na
kelele za mashabiki wala wachezaji atasimamiwa na Kamishna Bwire Manyama ambaye
ni mwamuzi mstaafu wa kimataifa.
Kwa upande wa waamuzi
wasaidizi wote wamechezesha mchezo wa watani hao wa Dar es Salaam mara tatu
ambapo Mkono ambaye ni mwalimu wa masomo ya sayansi Shule ya Sekondari Bungu
iliyopo Korogwe amechezesha michezo miwili ya ligi na mmoja wa ngao ya jamii.
Lila ambaye ni
miongoni mwa waamuzi chipukizi ambao CAF inawafuatilia na hivi karibuni ametoka Misri katika kozi
amezichezesha katika michezo ya ligi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment