MWENYEKITI
wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga ameteua wajumbe 12 akiwemo yeye mwenyewe watakaounda
kamati ya bodi ya ligi katika kikao kilichofanyika juzi.
Katika
taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari na Boniface Wambura ambaye ndiye Katibu
wa kamati hiyo inasema kamati itashughulikia uendeshaji na usimamizi wa Ligi
Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili
“Kamati
itaongozwa na Mwenyekiti mwenyewe, Shani Mligo ambaye ni Makamu Mwenyekiti,
Boniface Wambura ambaye ni Katibu, wajumbe ni Issa Batenga, Leslie Liunda na
Wakili Saleh Njaa,” alisema Wambura.
Wengine ni
Dk. Ellyson Maeja, George Malawa, Isaac Chanji, Baruan Muhuza, Mbakileki
Mutahaba na Ally Mayay.
Pia Sanga amewateua
Kanali Charles Mbuge ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting, na Abuu
Changawa (Majeki) kuingia kwenye kamati ya uongozi ya TPLB kwa mujibu wa Ibara
ya 28(vi) ya Kanuni za Uendeshaji za TPLB ambayo inampa nafasi ya kuteua
wajumbe wawili
No comments:
Post a Comment