SERIKALI
imeitaka Kampuni ya Maltchoice Tanzania kupunguza bei ya kulipia king’amuzi kwa
mwezi ili iwe rafiki kwa wateja na kuongeza watumiaji.
Hayo
yalisemwa jana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu katika sherehe ya kutimiza miaka
20 ya kutoa huduma nchini Tanzania iliyofanyika Dar es Salaam.
“Niwapongeze
kwa kufikisha mihongo miwili ya kutoa huduma, mimi ni mtumiaji wa king’amuzi
chenu na napenda kuangalia vipindi vya Eva na Maisha Magic Bongo kwani
inasaidia kupumzisha akili baada ya kuchoka,”
alisema
“Pia
niwapongeze kwa kuinua vipaji vya wasanii na wanamichezo hasa Simbu ambaye
mmewekeza sh. milioni 300 kwa sasa anafanya vizuri katika riadha lakini
muangalie namna ya kupunguza bei zenu ili ziwe rafiki kwa watumiaji,” alisema
Samia.
Pia Samia
aliwataka Maltchoice kuendelea kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo
ikiwa ni pamoja na kuwalipa wafanyakazi vizuri na kulipa kodi za serikali kwa
wakati serikali imeweka mipango thabiti ya kutoa ushirikiano kwa makampuni
binafsi.
Awali akizungumza,
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alisema
Maltchoice wamekuwa mfano wa kuigwa kwani wamekuwa wakitoa huduma bora na wameshiriki kuinua michezo.
“Kila mtu
ameona mchango wa Maltchoice na wanajali ubora na hivi karibuni walishiriki
tamasha la Jamfest lililofanyika nchini Uganda na kikubwa zaidi wamfadhili,
Felix Simbu ambaye anafanya vizuri katika riadha kimataifa na wamenidokeza 2020
wanatamani kuona wimbo wa Taifa ukiimbwa katika mashindano ya Olympiki,” alisema
Dk. Mwakyembe.
Awali
akieleza historia Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage
Chande, alisema walianza kufanya kazi Tanzania 1997 ikiwa na wafanyakazi saba
pekee na ilikuwa ikifanya kazi Dar es Salaam peke yake lakini sasa wapo mikoa
yote.
“Tulianza kufanyakazi tukiwa na wafanyakazi saba pekee na
ilikuwa tabu kutoa huduma mikoa ukizingatia pia teknolojia ilikuwa haijakuwa
kama sasa,”
“Ilichukua siku mbili hadi tatu kufunga dishi lakini jinsi
teknolojia ilivyokuwa kazi hiyo inafanyika katika dakika kadhaa tu hata kufikia
wateja mikoa ilikuwa shida na wateja wa mikoani ili kulipia ilibidi waende
benki halafu wanatuma fax ili waweze kuunganishiwa huduma,” alisema Chande.
Pia Chande alisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni
pale wanapotaka kubadilisha madishi baadhi ya wateja wanakataa wakidai
wanalotumia halina tatizo hivyo wanawapa elimu na hatimaye wanakubaliana.
No comments:
Post a Comment