NAIBU Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema msimu huu
wamepania kuhakikisha ubingwa wa Ligi Kuu unaondoka Dar es Salaam.
Angelina
ambaye ni mbunge wa Ilemela aliyasema hayo leo wakati akipokea basi kutoka
Kampuni ya GF Trucks ambao ni wadhamini wa Mbao FC.
“Niwashukuru
GF Trucks kwani msaada wao umekuja wakati muafaka na utachochea malengo yetu ya
kuondoa ubingwa wa ligi kuu kwa timu za
Dar es Salaam,” alisema
“Tuache
usimba na uyanga ndio mpira utakuwa na mnakumbuka Mbao FC wachezaji wengi
waliondoka tukabaki na wachezaji nane tu lakini tumeibua vipaji vingine na
vinafanya maajabu,” aliongeza Angelina Mabula.
Pia Angelina
Mabula alisema yeye ni mshabiki wa Yanga lakini linapokuja swala linalohusu
timu za nyumbani hasa mkoa wa Mwanza anakuwa upande wa Mbao ndio maana waliweza
kuzizuia Simba na Yanga zisiondoke na pointi tatu katika michezo yao.
Naye
Mkurugenzi wa GF Trucks Alijawah Karmali alisema anashukuru kutimiza moja ya
makubaliano yao waliyoingia na Mbao Agosti 25 mwaka huu
“Hatua hii
imetengeneza uhusiano mzuri kwa kampuni na wakazi wa kanda ya ziwa katika
kukuza masoko ya bidhaa zake na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla,”
alisema Karmali.
GF Trucks
iliingia mkataba na Mbao FC wenye thamani y ash 140,000,000 ambapo sh milioni
70,000,000 zimenunulia basi lenye uwezo wa kubeba watu 33 ambalo lilikabidhiwa
jana.
Hafla hiyo
pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi na wajumbe wa bodi ya
Mbao FC, Amoni Asabuki na Masalida Njashi pamoja wafanyakazi wa GF Trucks
&Equipments.
No comments:
Post a Comment