KOCHA wa
timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga amesema amepata mbinu za wapinzani wao
hivyo, wanakwenda kambini Misri kwa
tahadhari.
Mayanga na
kikosi cha wachezaji 21 kimeondoka leo nchini Misri kwa kambi ya
wiki moja kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la mataifa ya Afrika (Afcon)
dhidi ya Lesotho utakaochezwa Juni 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari kabla ya
kuelekea Misri Mayanga alisema watakuwa wanafanya mazoezi kwa tahadhari wakijiandaa kiufundi na kimbinu
kuwakabili wapinzani wao.
“Tumewaona
Lesotho ni wazuri, wamekuwa wakishambulia kwa pamoja na kuzuia kwa pamoja. Pia
ni timu inayojua kumiliki mpira,”alisema na kuongeza kuwa alifuatilia kupitia
mechi zake za mwaka jana ambapo wanaonyesha kupata matokeo mazuri.
Alizungumzia
sababu za kuchagua Misri kwa ajili ya kambi hiyo kwamba kuna hali ya hewa nzuri
inayofanana na Dar es Salaam na vile vile, kuna miundombinu bora kwa ajili ya
mazoezi.
Mayanga
alitaja sababu za kuwaacha wachezaji wawili Mwinyi Haji na Aggrey Morris na
nafasi zao kuchukuliwa na Gadiel Michael wa Azam na Nurdin Chona wa Tanzania
Prisons ni kutokana na mkanganyiko wa sheria na kanuni za Shirikisho la Soka
Afrika (CAF) baada ya Zanzibar kujiunga kuwa mwanachama.
Alisema bado
kuna hofu kwa jamii juu ya wachezaji wa
Zanzibar na Tanzania bara hivyo, ameona awaache kwanza mpaka jamii itakapoelimishwa sheria na kanuni
na nani anayehitaji kuchezeshwa.
Alisema
Zanzibar itaanza kushiriki michuano ya CAF
mwaka 2022 hivyo, kwa sasa kuna wachezaji ambao walianza kucheza Taifa
Stars wataendelea kuitumikia timu hiyo kama ambavyo sheria zinaelekeza. Lakini
kwa wachezaji pia, wanaweza kuchagua
timu ipi wachezee.
Pia,
alifafanua kuwa wachezaji ambao hawakuwahi kuitwa kuchezea Taifa Stars ndio
ambao wanaweza kuichezea Zanzibar heroes.
Waliokwenda
kambini ni makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga
SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar). Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni
Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto
wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael.
Walinzi wa
kati Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda
(Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) ilihali viungo wa kuzuia ni Himid
Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye hatasafiri na timu kwa
sasa.
Viungo wa
kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na Mzamiru
Yassin (Simba) wakati viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Yanga SC), Shiza
Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania).
Washambuliaji
Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden),
Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa
(Ruvu Shooting).
No comments:
Post a Comment