JANUARI inafika nusu na maana yake kwa watu wa soka ni kwamba dirisha
dogo la usajili limebakisha kama wiki mbili lifungwe.
dogo la usajili limebakisha kama wiki mbili lifungwe.
Klabu zinatafuta wachezaji wapya wa kuziba mapengo na kujiimarisha
wakati ligi nyingi zikiwa nusu mwendo.
Barcelona na Juventus
wanataka kumsajili kiungo wa Liverpool, Adam
Lalana (28), lakini inaelezwa kwamba wanakabiliana na ushindani kutoka
kwwa matajiri Paris Saint-Germain (PSG).
Lalana (28), lakini inaelezwa kwamba wanakabiliana na ushindani kutoka
kwwa matajiri Paris Saint-Germain (PSG).
Jose Mourinho na Manchester United wanataka kutoa pauni milioni 40 ili
kumpata kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko ili kuwazidi kete Chelsea
wanaomuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.
West Ham wanaofanya hovyo
msimu huu chini ya Slaven Bilic wanakaribia
kumnasa mshambuliaji wa Brentford, Scott Hogan kwa dili lenye thamani
ya pauni milioni 15, baada ya dili nyingine tatu kwa mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 24 kupigwa chini.
kumnasa mshambuliaji wa Brentford, Scott Hogan kwa dili lenye thamani
ya pauni milioni 15, baada ya dili nyingine tatu kwa mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 24 kupigwa chini.
Chelsea wanawapandia Middlesbrough kumpata mlinzi wao, Ben Gibson (23)
kama kusudio lao la kwanza kwa ajili ya kuziba nafasi ya nahodha John
Terry anayezeeka, lakini ambaye pia si ajabu akaenda China kiangazi
kijacho.
Habari nyingine zinasema Terry (36) hataondoka klabuni hapo kabla ya
mwisho wa msimu, mwenyewe akisema mawazo yake yamejikita kusaidia
klabu kutwaa ubingwa wa England.
Wengine wanasema Terry ameanza mazungumzo na bosi wa Bournemouth,
Eddie Howe, kuona uwezekano wa kuhamia huko, kwani angependa kubaki
England.
Kocha wa Sunderland, David Moyes anafikiria kumsajili kiungo wa
Everton, Tom Cleverley (27).
Mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi (23) ameambiwa kwamba hawezi
kuondoka Chelsea, licha ya Swansea na West Ham kumtaka mwezi huu. Ana
mtihani mgumu.
Bosi wa West Bromwich Albion, Tony Pulis yupo tayari kupeleka ‘mahari’
Crystal Palace ili kumnasa mshambuliaji Christian Benteke (26) na
anaweza kugharamia dili hiyo kwa kumuuza Saido Beraniho (23).
Kiungo wa Barcelona, Ivan Rakitic (28) anatakiwa na Manchester City
kuimarisha kikosi cha Pep Guardiola lakini wakuu wa Nou Camp
wanamwambia hawezi kuondoka hapo, walau Januari hii.
Bosi wa Crystal Palace, Sam Allardyce ‘Big Sam’ anakaribia kukamilisha
usajili utakaogharimu pauni milioni tatu wa beki wa kulia wa Arsenal,
Carl Jenkinson. Wanataka pia kumsajili beki wa kushoto wa Sunderland,
Patrick Van Aanholt (26).
Mabingwa wa Italia, Juventus wanamnyemelea kiungo wa Liverpool, Emre Can.
Arsenal wanasema hawatamruhusu nahodha na mlinzi wao wa kati, Per
Mertesacker (32) kuondoka wka mkopo mwezi huu, licha ya kutocheza hata
dakika moja msimu huu baada ya kuumia vibaya akiwa mazoezini.
Kocha wa Hull, Marco Silva amethbitisha kwamba kiungo wa Porto,
Evandro (30) anaweza kujiunga na klabu hiyo. Walipata kuwa pamoja
klabuni Estoril.
Swansea wamezungmza na beki wa pembeni wa Norwich, Martin Olsson (28),
wakishinikiza ajiunge nao Januari hii kuwaokoa kwenye eneo baya
walilojikuta msimu huu.
West Ham wamerudi Hull wakiwa na kitita bora zaidi, pauni milioni
tano, kwa ajili ya kumpata kiungo Mskochi mwenye umri wa miaka 29,
Robert Snodgrass alyefunga mabao 12 kwa klabu na taifa lake msimu huu.
Klabu ya Ufaransa, Lyon wamebisha hodi Manchester United ili
wawachukue washambuliaji wake, Memphis Depay (22) na Adnan Januzaj
(21) aliye kwa mkopo Sunderland.
Katika kujiimarisha, kocha Ronald Koeman anataka Everton kinda wa
miaka 17 wa Sheffield Wednesday, George Hirst. Koeman anataka
kumsajili kiungo wa Arsenal na England, Jack Wilshere aliye kwa mkopo
Bournemouth.
Mshambuliaji huyu ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Owls, David.
Arsenal wanakuna kichwa jinsi ya kuwapatia dili mpya wachezaji wao,
Alexis Sanchez na Mesut Ozil lakini wamekamilisha kazi kwa kuwatia
pingu ya muda mrefu mshambuliaji Olivier Giroud (30), mlinzi Laurent
Koscielny (31) na kiungo Francis Coquelin (25).
Barcelona wapo tayari kuchuana na mahasimu wao, Real Madrid ili
kumpata kiungo wa Tottenham Hotspur, Dele Alli (20).
Zipo habari kwamba kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino anatakiwa Barca
kuchukua nafasi ya Luis Enrique.
Mshambuliaji wa Manchester City, Wilfried Bonny (28) kutoka Ivory
Coast aliye kwa mkopo Stoke, amepewa ofay a mshahara wa pauni 210,000
bila kodi ili akacheze soka China.
Cio…
No comments:
Post a Comment