RAUNDI ya
pili ya Ligi Kuu ya Wanawake inatarajia kuanza leo katika viwanja vinne kwenye
miji tofauti vikiwaka moto.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Alfred Lucas alisema kundi B litakuwa na mechi mbili ambazo ni za Majengo FC
itacheza na Marsh AFC kwenye Uwanja wa Namufua Singida.
“Ligi Kuu ya
wanawake ilisimama kupisha usajili wa dirisha dogo hivyo kesho (leo) inatarajia
kuanza kwenye viwanja vya miji ya Bukoba, Singida, Iringa na Dar es Salaam,”
alisema Lucas
Mchezo
mwingine wa kundi B ni kati ya Panama FC na Sisterz ya Kigoma utakaochezwa
Uwanja wa Samora Iringa na Victoria Women ya Kagera wataialika Baobab FC kwenye
Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Kundi A
Mburahati FC itacheza na Viva ya Mtwara kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam
na kesho Evergreen itacheza na Fair Play kwenye Uwanja wa Karume na Mlandizi FC
wataikarisha JKT Queens kwenye Uwanja wa Mabatini Pwani.
JKT Queens
inaongoza kundi B ikiwa na pointi ikwa na 13 ikifuatiwa na Mlandizi yenye
pointi kumi, Evergreen yenye pointi tisa, Mburahati yenye pointi mbili, Viva
yenye pointi moja na Fair play ikiburuza mkia bila pointi.
Kundi B
linaongozwa na Sisterz yenye pointi 15, ikifuatiwa na Marsh yenye pointi kumi,
Panama yenye pointi nane, Baobab yenye pointi mbili na Victoria Women inaburuza
mkia ikiwa na pointi moja.
No comments:
Post a Comment