TANZANIA
imefanikiwa kutetea nafasi zake 18 za waamuzi wenye beji za Fifa kwa msimu wa
2017.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyowekwa kwenye www.fifa.com
inasema Tanzania imefanikiwa kupata beji 18, wanawake beji saba na wanaume 11.
Waamuzi wa
kati waliopata beji kwa upande wa wanaume ni Israel Mujuni, Nassor Mfaume,
Marthin Saanya, Elly Sasii ambaye amechukua nafasi ya Waziri Sheya ambaye
amestaafu kwa mujibu wa sheria.
Waamuzi
wasaidizi wanaume ni Josephat Bulal, Fernand Chacha, John Kanyenye, Kinduli
Mgaza, Frank Komba, Soud Lila na Samwel Mpenzu.
Kwa upande
wa wanawake wanaopuliza filimbi ni Florentina Zablon, Jonesia Rukyaa na
Mwanahamisi Matiku ambaye amechukua nafasi ya Sophia Mtogole ambaye alishindwa
kutetea beji yake.
Waamuzi
wasaizi wanawake ni Grace Wamala, Dalila Jafari, Hellen Mduma na Janet Balama
ambaye amechukua nafasi ya Kudra Omar ambaye alishindwa kutetea beji yake.
Kwa ukande
wa Afrika Mashariki na Kati, Sudan inaongoza ikiwa na waamuzi 28 ikifuatiwa na
Uganda yenye waamuzi 22, Rwanda yenye waamuzi 20 na Tanzania inashika nafasi ya
nne na waamuzi 18.
Burundi na
Kenya zikikabana kwenye nafasi ya tano zikiwa na waamuzi 16 kila moja, Somalia ina
waamuzi tisa na Sudan Kusini ina waamuzi nane.
Brazili
inaongoza kwa dunia ikiwa na waamuzi 40, ikifuatiwa na Spain yenye waamuzi 37
ikifuatiwa na Argentina yenye waamuzi 36, ujeruman waamuzi 33 na Misri inaongoza
kwa bara la Afrika ikiwa na waamuzi 32.
No comments:
Post a Comment