KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kipigo cha mabao
4-0 walichopata toka kwa Azam FC ni darasa kwa wachezaji kujua hawatakiwi
kudharau mechi hata kama wamefuzu.
Akizungumza na gazeti hili Mwambusi alisema wachezaji walicheza
wakijua wameshavuka kwenye hatua ya makundi na kustarehe na kuacha kuonyesha
juhudi uwanjani na kuacha njia wazi.
“Wachezaji wetu walicheza huku kichwani wakijua tumeshavuka
kwahiyo hakukuwa na haja ya kuweka nguvu zaidi lakini ni somo kwetu tunatakiwa
tucheze mechi zetu kwa uangalifu kwa sababu tumepoteza hii mechi tunakubali
matokeo,” amesema Mwambusi
Pia Mwambusi alisema wachezaji walistarehe na kuacha njia wazi Azam
wakacheza kwa nguvu na kupata mabao manne na kudai ni masikitiko lakini watarekebisha
makosa.
Naye kocha wa Azam
FC, Idd Cheche alisema walitumia mbinu ya kukaba viungo wa Yanga ndio maana
walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-0.
Akizungumza na
gazeti hili, Idd Cheche alisema Yanga wanategemea mipira ya pembeni kushambulia
hivyo mimi nikakaba wachezaji viungo wa Yanga wakashindwa kupata mpira.
“Yanga wanategemea sana kushambulia kupitia mipira
ya pembeni hivyo sisi tukaangalia wale wachezaji wachezaji ambao wanawachezesha
tukakamata sehemu ya kiungo tukauwa lengo lao,” alisema Cheche
Bao la
kwanza kwenye mchezo huo lilifungwa na nahodha John Bocco 'Adebayor' dakika ya
pili kwa shuti la mguu wa kushoto kufuatia mpira uliopanguliwa na kipa Deo
Munisha ambao ulipigwa na winga Joseph Mahundi bao lililodumu hadi mapumziko.
Azam FC
walilishambulia lango la Yanga kila mara na dakika ya 54 Yahaya Mohammed
aliipatia Azam bao la pili kwa kichwa baada ya kupokea krosi kutoka kwa
Abubakar Salum 'Sure boy.
Mahundi alifunga bao la tatu dakika ya 80 kwa shuti kali akiwa nje ya eneo la 18 baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Gadiel Michael Dida kuchupa bila mafanikio.
Akitokea benchi Enock Atta Agyei alihitimisha karamu ya mabao baada ya kufunga bao nne dakika ya 84 akitumia vyema makosa ya Geofrey Mwashiuya aliyeshindwa kuokoa krosi iliyopigwa na Mahundi.
Kwa matokeo hayo Azam imeongoza kundi B ikiwa na pointi saba huku Yanga wakishika nafasi ya pili baada ya kujikusanyia pointi sita.
Mahundi alifunga bao la tatu dakika ya 80 kwa shuti kali akiwa nje ya eneo la 18 baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Gadiel Michael Dida kuchupa bila mafanikio.
Akitokea benchi Enock Atta Agyei alihitimisha karamu ya mabao baada ya kufunga bao nne dakika ya 84 akitumia vyema makosa ya Geofrey Mwashiuya aliyeshindwa kuokoa krosi iliyopigwa na Mahundi.
Kwa matokeo hayo Azam imeongoza kundi B ikiwa na pointi saba huku Yanga wakishika nafasi ya pili baada ya kujikusanyia pointi sita.
Kwa matokeo
hayo Azam FC imeifunga Yanga mabao 38 na Yanga imeifunga Azam FC mabao 37 tangu
zianze kukutana Octoba 15, 2008 katika mechi za mashindano mbalimbali
walikutana.
Ushindi wa
mabao 4-0 wa Azam FC ni wa 10 sawa na Yanga ambao wameifunga 10 na kutoka sare
mara nane na kuwa na rekodi ya kuwa ndio timu pekee Tanzania inayoizidi Yanga
kwa matokeo.
Kabla ya mchezo
Yanga walikuwa wameizidi Azam FC kwa ushindi mmoja na mabao matatu kwenye
mashindano yote waliyokutana zikiwa zimelingana kila kitu.
Kwenye
Ligi Kuu zimecheza mara 17, Yanga imeshinda mara tano na Aza mara tano zimetoka
sare mara saba.
No comments:
Post a Comment