UONGOZI wa Mbeya City umethibitisha uhamisho wa kimataifa wa kiungo mshambuliaji, Mrisho Ngassa toka klabu ya Fanja FC ya Oman.
Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Mbeya City, Mussa Mapunda amethibitisha kupokea ITC kutoka shirikisho la soka la Oman
“Tumepata ITC, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa shirikisho la soka nchini,TFF, chama cha mpira cha Oman, hakika wamefanya kazi kubwa kufanikisha kupatikana kwa ITC na watendaji wote wa timu yetu, tumekuwa na mawasiliano mazuri muda wote mpaka tumefanikiwa,” alisema Mapunda.
Pia Mapunda alisema kuchelewa kufika kwa ITC hii hakukuwa na msuguano wowote baina ya klabu hizi mbili kilichokuwa kinatokea ni tofauti ya wakati na siku za ufanyaji kazi kwenye ofisi kulingana na taratibu za nchi hizi mbili.
Ngassa alijiunga na Mbeya City kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa pamoja na wachezaji wengine kumi waliosajiliwa .
Kabla ya kusajiliwa Fanja FC, Ngassa ambaye amewahi kuchezea Simba, Yanga na Azam FC alikuwa akicheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Free State ya Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment