Kikosi kilichoanza cha Manchester uniteddhidi ya Leverkusen huko Ujerumani leo usikuKocha wa Manchester United boss David Moyes akitoa maelekezo hapa Mchezaji wa Manchester United Antonio Valencia akishangilia bao lake Kocha wa zamani wa United Sir Alex Ferguson nae alikuwepo kwenye watazamaji kwenye UEFA Champions League Grupu A kati ya Bayer Leverkusen na Manchester United huko BayArena Ujerumani.Giggs akimpongeza Jonathan Evans baada ya kufunga bao kipindi cha pili dakika ya 65.Manchester United wakitandaza soka safi bila Mshambuliaji wao Van Persie huko Ujerumani BayArena wameifunga timu ya Bayer Leverkusen bao 5-0. Bao za United zimepatikana kipindi cha kwanza na cha pili. Bao la kwanza likifunguliwa na Antonio Valencia katika dakika ya 22, Bao la pili wakijifunga wao wenyewe kupitia mchezaji wao Emir Spahic katika dakika ya 30. Mchezaji Jonathan Evans akifunga bao safi la tatu dakika ya 65 kipindi cha pili baada ya mpira kutemwa kizembe kwenye eneo la box la lango la Bayer Leverkusen. Chris Smalling akifunga bao baada ya kupewa mpira kupitia kona iliyopigwa na Wayne Rooney na kuuzima vizuri na kutupia katika dakika ya 77 na bao la tano likifungwa na mhezaji matata Nani katika dakika ya 88. Ushindi huu unawaweka pazuri kwa kuongoza kundi "A" wakiwa na alama 11.
Wachezaji wa Manchester United wakipongezana baada ya Smalling kufunga bao katika dakika ya 77 dhidi ya wenyeji Bayer Leverkusen huko Germany, United imeshinda kwa jumla ya mabao 5-0.
Wayne Rooney pamoja na kutofunga leo ametoa pasi zilizosabaisha mabao manne leo hii!! kazi yake leo ilikuwa kusindikiza pasi safi zikiwemo kona!!
Antonio Valencia ndie alieanza kuliona lango la wenyeji baada ya kupata krosi safi kutoka kwa Wayne Rooney na kufanya 1-0.
Emir Spahic kwenye patashika na kujifunga bao!
Jonny Evans (kushoto) akikimbizwa huku akishangilia bao lake
Chris Smallingakitupia la nne
Nani akitupia la mwisho la dfakika za lala salama dakika ya 88 na kufanya 5-0
Wakipongezana kwa kazi nzuri hapa !
VIKOSI:
Bayer Leverkusen: Leno, Spahic, Omer Toprak, Donati, Reinartz (Hegeler 70) Rolfes, Bender (Kohr 81), Can, Castro, Son (Derdiyok 70), Kiessling.Subs not used: Lomb, Stafylidis, Wollscheid, Kruse.
Booked: Kohr.
Manchester United: De Gea, Smalling, Ferdinand, Evans, Evra (Buttner 70), Giggs, Jones, Valencia (Young 80), Kagawa, Nani, Rooney (Anderson 80).
Subs not used: Lindegaard, Cleverley, Hernandez, Welbeck.
Goals: Valencia 22, Spahic (OG 30), Evans 65, Smalling 77, Nani 88.
Ref: Svein Oddvar Moen.
Man of the match: Wayne Rooney
No comments:
Post a Comment