Mshambuliaji
mwenye mafanikio na soka la Tanzania na pia mwenye rekodi pekee ya
kucheza timu kubwa tatu nchini ambazo ni Yanga,Azam na Simba,Mrisho
Khalifani Ngassa hata hivyo ameweza kuvitumikia vilabu vya kanda ya
Ziwa,Scad Magu ya Magu,Toto African ya Mwanza na Kagera Sugar ya Kagera
kwa nyakati tofauti ameamua kuvunja mkataba wake na klabu ya Free State.
Ngassa alikutana uongonzi wa timu hiyo
na kukaa kikao kizito chini ya Meneja,Rantsi Mokoena hivyo pande zote
mbili zilikubaliana kuwa mchezaji huyu avunje mkataba na wao kama timu
wanaheshimu maamuzi ya mchezaji huyu mwenye rekodi ya kuwa mfungaji bora
wa michuano ya klabu bingwa Afrika akiwa na timu ya Yanga.
Meneja wa Free State,Rantsi Mokoena.
“Ni kweli Ngassa tumekubaliana naye
kuvunja mkataba kwani alikuwa na mashiko yake na yalikuwa na msingi
hivyo tunamshukuru kwa muda ambao tumekaa naye alikuwa mchezaji mzuri
kwetu ameweza kutusaidia hivyo tunamtakia maisha mema na
mafanikio”alisema Mokoena.
Hoja kubwa ambayo inasemekana Ngassa
kuamua kuvunja mkataba na timu hiyo ni kwamba Free State hawana malengo
na kushinda taji na yeye malengo yake ni kutwaa makombe mbalimbali wao
wapo kwa ajili ya kushiriki Ligi tu bila kuwa na malengo na mafanikio
hii ndio hoja kubwa.
Kikosi cha Free State.
Free State tayari wameshaingia na
Mkataba na mshambuliaji hatari wa zamani wa Yanga na Simba,Hamis
Kiiza,walioingia naye kwa mkataba wa miaka minne pengine Ngassa ameamua
kumkimbia Kiiza kutokana na uimara wa kufumania nyavu,Kiiza alikuwa
mchezaji wa Simba msimu uliopita na aliweza kufunga magoli 19 nyuma ya
mfungaji bora wa ligi Amis Tambwe ambaye alifunga magoli 21 akiwa na
Yanga na mwaka huu wekundu wa msimbazi wameweza kuachana naye kutokana
kuwa na nidhamu mbovu.
Add caption
Mshambuliaji wa zamani wa Simba,Hamis Kiiza.
Hata hivyo huu umekuwa utamaduni wa
wachezaji wa Tanzania kuweza kupata nafasi za kucheza soka la kimataifa
wanacheza msimu mmoja mara unasikia wanarudi nyumbani kwa sababu ambazo
hazina mashiko mfano mzuri Haruna Moshi Boban alikuwa anacheza nchini
Sweden katika timu ya Malmo inayoshiriki ligi ya nchi hiyo naye aliamua
kuvunja mktaba na pia mlinzi wa Azam,Shomari Kapombe alikuwa nchini
Ufaransa timu ya Daraja la pili naye hivyo hivyo na wengine.
Ukiachana na Samatta na Ulimwengu ambao
wanacheza soka la nje lakini wachezaji waliobaki pengine bado
hawajazaliwa kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa wapo kwa ajili ya
kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania na pia kucheza Simba,Yanga na Azam
ndio ndoto zao,swali la kujiuliza baada ya kuvunja mkataba Ngassa
atarudi Yanga au kuna timu kapata nje ya Afrika Kusini Ngoja tuone.
NMB YAPELEKA ELIMU YA FEDHA KWA MAELFU YA VIJANA
-
Benki ya NMB imesisitiza umuhimu wa kupeleka elimu ya fedha kwa umma
sambamba na kupanua huduma rasmi za kifedha, ikisema ujumuishaji wa kifedha
unahita...
Leadership and Teamwork, Defined by the Serengeti
-
If you want a masterclass in leadership, style, and pure majesty, you don't
look to a boardroom you look to the plains of the Serengeti.
Watching an e...
Uchumi : Rais Samia Aipa BOT Dira Mpya
-
Na Janeth Raphael MichuziTv
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameielekeza
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuongeza uwezo wa kuc...
WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS
-
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen
Wasira, Leo Machi 27, 2026, Mjini Bunda Mkoa wa Mara alipokuwa akiweka
jiwe la ms...
Post a Comment