Wednesday, July 20, 2016
WACHEZAJI 10 WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA
Majina 10 ya wanasoka wanaowania tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya yamewekwa hadhari na sirikisho la soka barani humo UEFA baada ya kufanya mchujo kutoka kwenye jumla ya majina 37 yaliyokuwa katika kinyang’anyiro hicho.
Tuzo hiyo inatarajiwa kutolewa tarehe 25 mwezi ujao huku nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo akipewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na kutwaa mataji mawili makubwa yanayoandaliwa na UEFA katika mwaka huu.
Hi ndiyo orodha ya majina 10 yanayowania tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya msimu wa 2015/16
Cristiano Ronaldo (Real Madrid & Ureno)
Gareth Bale (Real Madrid & Wales)
Gianluigi Buffon (Juventus & Italia)
Antoine Griezmann (Atlético Madrid & Ufaransa)
Toni Kroos (Real Madrid & Ujerumani)
Lionel Messi (Barcelona & Argentina)
Thomas Müller (Bayern München & Ujerumani)
Manuel Neuer (Bayern München & Ujerumani)
Pepe (Real Madrid & Ureno)
Luis Suárez (Barcelona & Uruguay)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment