Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 23, 2016

SAM ALLARDYCE APEWA NAFASI KUIFUNDISHA ENGLAND

Sam Allardyce apewa Timu ya Taifa ya England.
SAM ALLARDYCE, mwenye Miaka 61, ameteuliwa rasmi kuwa Meneja Mpya wa England na kusaini Mkataba wa Awali wa Miaka Miwili baada ya Klabu yake Sunderland kukubali kulipwa Fidia.

Allardyce, maarufu kama Big Sam., anamrithi Roy Hodgson alieondoka mara baada ya England kutupwa nje ya EURO 2016 walipufungwa na Iceland kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

Mechi ya kwanza kwa England ambayo Allardyce ataiongoza ni hapo Septemba Mosi kwenye Mechi ya Kirafiki dhidi ya Mpinzani ambae hajatajwa.

Taarifa ya FA, Chama cha Soka England, imesema lengo kuu la Meneja huyo mpya ni kuhakikisha England inafuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Jukumu linguine la Allardyce ni kumsaidia Mkurugenzi wa Ufundi wa FA Dan Ashworth kuboresha Programu za Makocha kwa Timu kuu za England na zile za Vijana.

Mechi ya kwanza ya Mashindano rasmi ni ile ya Makundi ya kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za 2018 hapo Septemba 4 dhidi ya Slovakia.

Allardyce, Meneja wa zamani wa Klabu za Bolton, Newcastle, Blackburn na West Ham, anakuwa ni Meneja wa 14 wa kudumu wa Timu ya Taifa ya England.

No comments:

Post a Comment