Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis amebainisha kuwa walikataa ofa ya euro milioni 60 na wachezaji wawili au watatu kutoka Atletico Madrid kwa ajili ya mshambuliaji Gonzalo Higuain.
Higuain mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akitajwa kuwindwa na klabu za Juventus na Arsenal huku akiwa amewekewa kitenzi cha euro milioni 94 katika mkataba wake.Hata hivyo, Atletico ambao wanatafuta mshambuliaji mpya kiangazi hiki ndio wamekuwa wa kwanza kutuma ofa yao kwa Napoli.
De Laurentiis amesema Atletico ndio timu pekee iliyotuma ofa yao, na kutoa ofa ya euro milioni 60 na wachezaji wawili au watatu.
Juventus pia wameripotiwa kuanza mazungumzo wiki hii lakini De Laurentiis amepuuza tetesi hizo akidai kuwa hadhani kama wanaweza kuwauzia wapinzani wao.
You might also like:
No comments:
Post a Comment