Kumekuwa na taarifa
za upotoshaji kuhusu uratibu na ushiriki wa klabu za Tanzania katika mashindano
ya kimataifa hususani ushiriki wa Young Africans SC katika mashindano ya Kombe
la Shirikisho kwa msimu wa 2015/2016.
Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), limekuwa likitoa kila aina ya msaasa uliowezekana
kuisaidia klabu za Young Africans na Azam ambazo ziliwakilisha nchi katika
mashindanmo ya kimataifa. Kwa upande wa Young Africans awali walishiriki Ligi
ya Mabingwa Afrika na upande wa Azam ilishiriki Kombe la Shirikisho Barani
Afrika.
Mtakumbuka, Azam FC
ilitolewa na Esperance ya Tunisia katika michuano hiyo na kwa upande wa Young
Africans iliposhindwa kufuzu kwa hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika,
ikashushwa na kucheza na Esperanca Sagrada ya Angola na kuitoa hivyo kufuzu kwa
hatua ya Nane Bora ya Kombe la Shirikisho au kwa lugha nyingine, hatua ya
Makundi. TFF ikaendelea kuisaidia Young Africans kuhakikisha inashiriki vema
katika mashindano hayo.
Sasa, Aprili 21,
2016 Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilitoa waraka kwa timu
zilizokuwa zinacheza kuwania kuingia hatua ya Makundi (Ligi ya Mabingwa Afrika
na Kombe la Shirikisho) kupeleka majina ya maofisa watakaohudhuria warsha ya
namna ya kuratibu mechi hizo kuelekea fainali. Kadhalika walitakiwa kupeleka
vivuli (photocopies) vya hati zao za kusafiria.
Maofisa walihitajika
ni meneja wa timu, daktari wa timu na ofisa habari wa timu. Taarifa hiyo
ilikuja kabla ya Young Africans kucheza na Esperanca ya Angola. TFF
iliwaataarifu Young Africans kwa kuwataka kutuma nyaraka hizo kati ya Aprili 26
na Aprili 28, 2016.
Lengo la warsha
ilikuwa ni kujadili maswala ya uratibu, ufundi, udhamini na kanuni za
mashindano. CAF ilijitolea kugharamia usafiri, malazi na gharama zote kwa watu
watatu kutoka Young Africans SC
Taarifa hizi na hata
ukumbusho (reminders) zilipelekwa kwa baruapepe, simu na hata kuonana ana kwa
ana kwa Katibu Mkuu wa Young Africans, Ofisa Habari na Viongozi wengine wa
klabu.
Maofisa wa TFF kwa
nyakati tofauti tofauti waliwasihi Young Africans na pia kuwakumbusha kutuma
majina CAF na vivuli vya hati hati ya kusafiria, lakini kwa sababu wanazoweza
kuzielezea wenyewe kwa nini hawakupeleka majina.
Mei 22, 2016 ikiwa
ni siku mbili kabla ya warsha kuanza hapo Mei 24, 2016, Kaimu Katibu Mkuu wa
Young Africans, Bwana Baraka Deusdedit alituma majina CAF yakiwa hayana vivuli
yaani photocopies vya hati ya kusafiria.
Siku moja kabla ya
washiriki kuanza kuwasili Cairo, Misri, Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans
alituma nyaraka kama zilivyotakiwa na wakatumiwa tiketi tatu (3) na CAF. Pamoja
na tiketi kuletwa Young Africans bado watu hao hawakusafiri wakidai klabu
haijatoa ruhusa.
Maofisa wa TFF
wamekuwa wakifanya kazi mpaka muda wa ziada wakiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa
Young Africans, Baraka Deusdedit ili timu iweze kushiriki vema pamoja na
upungufu wa kiutawala ndani ya sekretarieti yake yanayojidhihirisha wazi.
Masuala yote
yanayolalamikiwa na Ofisa Habari wa Young Africans, yaliyotolewa kwa timu zote
kwenye semina ya Cairo, Misri.
TFF itaendelea
kuvitembelea kusaidia klabu kujenga weledi kupitia mradi wa leseni za klabu na
vilevile kuratibu ushiriki wa mashindano mbalimbali.
Hata hivyo, TFF
haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa maofisa wa klabu wanaochafua jina la
shirikisho ili kuficha madhaifu yao ya kiutawala (Administrative
inefficiencies).
No comments:
Post a Comment