KOCHA wa Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania
umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Bakari Shime, amejigamba kuondoka na
pointi tatu kwenye mchezo wao dhidi ya Shelisheli utakaochezwa Uwanja wa Taifa,
Jumapili hii.
Akizungumza
na gazeti hili Shime alisema timu yake ameiandaa vyakutosha kwani imepata mechi
za kimataifa za kirafiki hali iliyomwezesha kukisuka vema kikosi hicho.
“Naamini
kwa maandalizi haya tutasonga mbele kwenye hatua inayofuata na vijana wana ari
ya kwenda Madgascar 2017 kwenye fainali za mashindano haya”, alisema Shime.
Mchezo huo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za
Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 utachezeshwa na
waamuzi toka Ethiopia ambao ni Belay Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati na
wasaidizi wake ni Tigle Belachew na Kinfe Yilma Kinfe huku mwamuzi wa akiba
akiwa ni Lemma Nigussie na Kamishna wa
mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys iliingia kambini Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa
Jumapili na marudiano ni Shelisheli Julai 2, 2016, endapo itafuzu hatua hii
itakutana na timu ya Vijana ya Afrika Kusini.
Naye nahodha wa timu hiyo, Issa Makamba amesema wapo
tayari kupambana na anaamini ushindi ni wao huku akiwataka mashabiki kuja
kuwashangilia.
No comments:
Post a Comment