MEJA wa jiji
la Dar es Salaam, Isaya Mwita, leo anatarajiwa kufungua mashindano ya ngumi za
ridhaa ya mkoa wa Dar es Salaam maarufu kama Meya Cup.
Mashindano
hayo ambayo yanashirikisha timu toka kwenye taasisi za ulinzi na usalama, wilaya
za mkoa wa Dar es Salaam na timu mwaliko toka nje ya nchi yameanza jana kwa
mabondia kupima afya na uzito na yatafika tamati Juni 25.
Akizungumza
na mtandao huu, Mwenyekiti wa Chama Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam,
Akaroly Godfrey alisema maandalizi yote yamekamilika na timu mwaliko
zimewasili.
"Maandalizi
yamekamilika na kesho (leo) Mstahiki meya wa jiji, Mwita ambaye mashindano yanabeba cheo chake atakuwa
mgeni rasmi na atatungulia mashindano saa tisa alasiri", alisema Akaroly.
Pia Akaroly
alisema timu zinazoshiriki ni Ilala, Kinondoni, Temeke, Ngome, JKT, Polisi
Baracks, Mombasa na Nairobi kaunti na timu ya jeshi la Maji toka Nigeria.
Wakati wa
zoezi la kupima uzito mabondia walikuwa wakitambiana huku kila mmoja akijigamba
kuchukua kombe hilo jambo ambalo linaonesha mashindano ya mwaka huu yatakuwa na
msisimko.
No comments:
Post a Comment