Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, June 15, 2016

RUSSIA YATIMULIWA EURO 2016 NA FAINI JUU

Russia itatimuliwa kwenye Euro 2016 kama Mashabiki wao wataleta fujo katika Mechi zilizobaki.

UEFA imeamua kuipa Russia Adhabu iliyositishwa ya kuifukuza kutoka EURO 2016 na pia kuitwanga Faini ya Euro 150,000 kutoka na vurugu za Mashabiki wao wakati wa Mechi na England huko Marseille, France hapo Juzi.
Mbali ya Adhabu hiyo ya UEFA, France, ambao ndio Wenyeji wa Fainali za EURO 2016, wameamua kuwafukuza Nchini kwao baadhi ya Mashabiki wa Russia.
Adhabu hizo za UEFA zilizotolewa Leo zinahusu matukio tu ya ndani ya Uwanja na Russia imepewa nafasi ya kukata Rufaa.
Lakini Waziri wa Michezo wa Russia, Vitaly Mutko, amesema hawatakata Rufaa.
Juzi Polisi wa France walidai lipo genge maalum la Warusi 150 waliosukwa kuleta fujo.

Jana Masahabiki 6 wa England walihukumiwa Vifungo kutokana na fujo za Mjini Marseille ambapo Watu 35 walijeruhiwa na 20 kukamatwa.
Mbali ya hatua hizo za Adhabu, bado upo wasiwasi mkubwa wa kulipuka fujo nyingine kati ya Mashabiki wa Russia na England ambazo zipo Kundi moja kwenye EURO 2016 kwani Russia wanacheza Jumatano na Slovakia huko Lille na England wanacheza Alhamisi na Wales huko Lens Miji ambayo ipo jirani na upo uwezekano Mashabiki hao kukutana.

Hata hivyo, France imeamua kuongeza hadi kufikia Polisi 2,400 katika sehemu hizo na pia Pombe kupigwa marufuku.

No comments:

Post a Comment