Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 16, 2016

KAPOMBE MCHEZAJI BORA WA MWAKA AZAM FC



BEKI wa Azam FC, Shomari Kapombe, amechaguliwa na mashabiki kuwa mchezaji bora wa timu hiyo kwa msimu uliopita.
Kwa mujibu wa habari iliyowekwa kwenye mtandao wa Azam FC, inasema zoezi la kumtafuta mchezaji wa kutwaa tuzo hiyo liliwahusisha wachezaji wengine sita.
Mashabiki  walipiga kura kupitia akaunti ya Azam FC kwenye mtandao wa kijamii wa facebook ambapo Kapombe aliwabwaga wapinzani wake watano kwenye kinyang’anyiro.
Wachezaji waliokuwa wanashindanishwa  ni nahodha msaidizi,  Himid Mao, beki Pascal Wawa, kipa Aishi Manula na washambuliaji Farid Mussa na Ramadhan Singano ‘Messi’.
Kapombe ametwaa tuzo hiyo baada ya kujizolea kura 203 kati ya zote 560 zilizokubaliwa, akifuatiwa na Aishi aliyepata kura 125, Farid  alipata kura 95, Singano kura 48, Himid alipata 45  na Wawa alipata kura 44.
Jumla ya kura 710 zilipigwa na mashabiki, lakini ni kura 560 tu zilizokubaliwa huku kura  150 ziliharibika baada ya wapigaji kukiuka masharti kwani kila shabiki alitakiwa kupiga kura kwa jina moja tu.
Mbali na tuzo hiyo ya mashabiki, Kapombe pia alifanikiwa kuwa mchezaji pekee wa Azam FC aliyepata tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari inayotolewa na mdhamini wa Ligi Kuu, Kampuni ya Vodacom.
Kapombe ameweka  rekodi ya kuwa beki pekee wa ligi kwa msimu uliopita  kwa kufunga mabao  nane na katika mechi zote ilizocheza Azam FC amefunga mabao 12 na kutoa pasi saba za mwisho.
Kapombe alicheza dakika 3188 msimu uliopita katika mechi zote ilizocheza Azam FC, lakini mwishoni hakufanikiwa kumaliza vema msimu baada kuugua ugonjwa wa kuziba mishipa ya damu katika mapafu na kukosa sehemu iliyobakia ya msimu lakini  afya yake sasa inaendelea vema .


No comments:

Post a Comment