Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 2, 2016

RASHFORD NA STURRIDGE NDANI YA KIKOSI CHA ENGLAND EURO 2016

LEO Kocha wa England Roy Hodgson atatangaza rasmi Kikosi chake cha Wachezaji 23 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2016 zinazoanza huko France hapo Juni 10.
Gumzo kubwa huko England ni kama Straika wa Liverpool Daniel Sturridge atabaki kwenye Timu na Chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford kuwemo.
Sturridge amekuwa akiandamwa na maumivu ya mara kwa mara na hilo pia lilimfanya aikose Mechi ya Ijumaa England ilipoifunga Australia 2-1 huku Kinda Marcus Rashford akianza Mechi yake ya kwanza kabisa kwenye Kikosi cha England na kupiga Bao la Kwanza.
Lakini Jana Sturridge alijumuika na wenzake wa England Mazoezini wakiwepo Wachezaji wote wa 25 wa England waliobaki baada ya Kiungo wa Man City Fabian Delph kujiondoa Kikosini akijiuguza Nyonga.
Leo Hodgson anapaswa kupunguza Wachezaji Wawili ili awasilishe rasmi UEFA Wachezaji 23 kwa ajili ya EURO 2016.

Kama angekuwa fiti kwa Asilimia 100, kusingekuwa na mjadala kuhusu Sturridge kuwemo Kikosini lakini majeruhi ya mara kwa mara yamemfanya Straika huyo wa Liverpool aichezee England Dakika 58 tu tokea Septemba 2014.
Hilo limetoa mwanya mkubwa kwa Kinda wa Man United Marcus Rashford apate fursa ya kwenda France kwenye EURO 2016 hasa baada ya Ijumaa iliyopita ya kuwa Kijana mdogo kabisa kuifungia England Bao katika ya kwanza tu tangu 1938.
ENGLANDMECHI ZA LEO HII
Ratiba/Matokeo:
Mei 2016
Kirafiki
Jumapili Mei 22

England 2 vs Turkey 1

Ijumaa Mei 27

England 2 Australia 1

Juni 2016
Alhamisi Juni 2
2145 England v Portugal

EURO 2016 Kundi B
Jumamosi Juni 11

2200 England v Russia

Alhamisi Juni 16
1600 England v Wales

Jumatatu Juni 2
2200 Slovakia v England

No comments:

Post a Comment