RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania, Jamal Malinzi
ametuma pongezi kwa Michael Wambura kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama
cha Soka mkoa wa Mara na Athuman Kambi kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama
cha soka mkoa wa Mtwara.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred
Lucas, alisema Malinzi amesema ana imani na viongozi hao kuwa wataendeleza soka kwenye
mikoa yao.
"Rais wa TFF amesema ana imani na viongozi
waliochagulia na kusema watasimamia vema soka kwenye mikoa yao kwani ni
viongozi wapenda soka", alisema Lucas.
Pia Lucas alisema uchaguzi huo umefanyika kulingana na
katiba na kalenda ya uchaguzi.
Kambi alikuwa
anatetea nafasi yake wakati Wambura
aliyewahi kuwa katibu mkuu wa chama cha soka nchini, FAT, sasa hivi Shirikisho
soka nchini, TFF alikuwa mgombea pekee.
Wambura
alishawahi kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo Urais wa Simba, lakini
aliondolewa kwa kuvunja kanuni za uchaguzi na wakati mwingine alidaiwa kukosa
sifa
No comments:
Post a Comment