MWENYEKITI
wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la
Soka Tanzania, (TFF), Aloyce Komba, amejiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi wa
klabu Yanga uliopangwa kufanyika Juni 25 , mwaka huu.
Hatua hii
imekuja baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kumtuhumu kumhujumu hivyo
anakaa pembeni kupisha uchunguzi
Akizungumza
na wandishi wa habari leo, Komba alisema Manji anasema nahusika kupanga
mikakati ya kupewa rushwa ili akate jina
lake na tuhuma hizi kwake ni nzito ukizingatia taaluma yake ya sheria.
“Manji ananituhumu
mimi kupanga mikakati ya kupewa rushwa ili nikate jina lake, tuhuma hizi kwangu
ni nzito ukizingatia taaluma yangu ya sheria, sitaki kuwa chanzo cha mgogoro
Yanga”, alisema Komba
Pia Komba
alisema wanasheria nguli Said el Maamry, Alex Mgongolwa, Mapande na baadhi ya wabunge ni watu
anaowaheshimu na wamemshauri juu ya suala hili hivyo kwa busara ameamua kukaa
pembeni uchaguzi ufanyike.
“Sauti zinazosemwa sizitambui, sizijui, halafu
najiuliza wanapanga kwa manufaa ya nani
? kwanini Manji katishika kuchukua fomu TFF wakati ameonyesha uwezo mkubwa wa
kuongoza Yanga?”, alihoji Komba.
Komba
alisema alitegemea Manji angemrahisishia kazi lakini matokeo yake anachafuka
kwa vitu ambavyo si vya kweli.
Mchakato wa
uchaguzi TFF unaendelea chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili Domina Mideli.
No comments:
Post a Comment