SHIRIKISHO la soka Afrika (CAF) leo limepanga droo
ya hatua ya makundi ya michuano yake ambapo Yanga inayoshiriki kombe la
Shirikisho Afrika imepangwa kundi moja na TP Mazembe ya DR Congo.
Mazembe imejizolea umaarufu nchini hasa baada ya
kuinyanyasa Simba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2011.
Lakini pia Watanzania wamekuwa wakiifuatilia
kutokana na kusajili wachezaji wawili wa kitanzania Mbwana Samatta ambaye kwa
sasa anacheza Ugiriki na Thomas Ulimwengu ambaye bado yupo Mazembe.
Kwa mujibu wa droo ya CAF jana mchana, Yanga
imepangwa kundi B na Mazembe, Mo Bejaia ya Algeria na Modeama ya Ghana.
Yanga ilifika hatua hiyo baada ya kuiondosha Sagrada
Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1 katika hatua ya 16 ya michuano hiyo
ya Shirikisho baada ya kuondolewa na Al Ahly ya Misri kwenye Ligi ya Mabingwa.
mechi za makundi zinatarajiwa kuanza kuchezwa mwezi ujao.
Kwa upande wa kundi B zipo timu za Kawkab Athletic,
Fath Union Sports za Morocco, Etoile du Sahel ya Tunisi na Ahly Tripoli ya
Libya.
Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Zesco ya Zambia
imepangwa kundi moja na Al Ahly ya Misri, Asec Mimosas ya Ivory Coast na Wac ya
Morocco. Kundi B lina timu za Enyima ya Nigeria, Zamalek ya Misri, Es Setif ya
Algeria na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment