Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeteua
waamuzi 40 watakaochezesha Ligi ya Mabingwa Mikoa (RCL) inayoanza leo
Mei 23 katika vituo vinne tofauti hapa nchini.
Ligi hiyo inayoshirikisha timu 27, imegawanywa katika makundi manne
ambako bingwa katika kila kundi atapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili
msimu wa 2016/17 ngazi ya taifa kabla ya kutafuta nafasi ya kucheza
Ligi daraja la Kwanza msimu wa 2017/18.
Timu tano zitapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili ambako mbali ya
washindi katika vituo vyote vinne, mshindwa bora katika vituo vya
Njombe, Morogoro na Singida nayo itapanda daraja kwa kuangalia vigezo
vya wingi wa pointi, wastani wa mabao, mabao kufunga na mabao ya
kufungwa. Kituo cha Kagera hakijajumuishwa kwa kuwa kina timu shiriki
sita.
Waamuzi walioteuliwa kuchezesha ligi hiyo kwa kituo cha Njombe ni
Elasto Msaliwa, Klement Manga, Mashaka Lulambo, Lazaro Mbogoro, Michael
Mkongwa, Alex Chitalula, Maulid Makiwa, Michael Kilango, Edina Ndelwa na
Haidal Kisingile.
Timu zinazoshiriki ni Mkali Stars ya Ruvuma, Mtwivila (Iringa), Sido
FC (Mbeya), Jangwani FC ya Rukwa, Nyundo FC ya Katavi, Mawezi ya
Morogoro na Zimamoto ya Ilala, Dar es Salaam.
Kituo cha Morogoro walioteuliwa ni Athuman Lazi, Mohammed Theophil,
Seleman Kinugane, Fikiri Yusuph ‘Magari’, Nicolaus Makangara, Mwarabu
Mumba, Emmanuel Muga, Herry Shao, Shaban Juma na Makongo Katuma na timu
zinazoshiriki ni Stend FC ya Pwani, Mbuga FC (Mtwara), Namungo
FC(Lindi), Muheza United ya Tanga, Stand Misuna FC ya Singida,
Makumbusho ya Kinondoni na Sifa Politan SC ya Temeke, Dar es Salaam.
Kituo cha Singida wako Meshack Suda, Abdallah Mwinyimkuu, Sarah
Bongi, Lucas Mathias, Amani Mwaipaja, Siyachitema Kawinga, Theophil
Tegamaisho, Shaaban Msangi, Aboubakar Irume na Frederick Ndahani na timu
shiriki ni Veyula FC (Dodoma), Pepsi SC (Arusha), Kitayosce FC
(Kilimanjaro), Stand FC (Tabora), Murusagamba FC (Kagera), Fire Stone
(Manyara) na Tomato FC (Njombe).
Kituo cha Kagera walioteuliwa ni Jonesia Rukyaa, Jamada Ahmada,
Ringston Rwiza, Grayson Buchard, Grace Wamala, Edgar Lyombo, Yahaya
Juma, Adrian Karisa, Getrude Kahawa na Ahmada Simba na timu shiriki ni
Geita Town Council Fc (Geita), Gold Sports Academy (Mwanza), Kabela City
(Shinyanga), Ambassador FC (Simiyu), Igwe FC (Mara) na Mashujaa
(Kigoma).
No comments:
Post a Comment