Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 23, 2016

WEMA SEPETU AZINDUA HUDUMA YAKE IITWAYO WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akizindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akimpa mkono wa pongezi msanii wa filamu hapa nchini,Wema Sepetu kwa kubuni huduma ya kisasa kabisa WEMA MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar

Mwanadada Wema Sepetu akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye kabla ya uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuzindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar
Msanii mahiri wa filamu hapa nchini Maadam Wema Sepetu akizunguma mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),jioni ya leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar kabla ya kuzindua huduma yake WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION,ambayo itakuwa ikijumuisa matukio yake yote sambamba na video mbalimbali yatakayowekwa kwenye mfumo wa teknolojia ya kisasa kupitia simu za mikononi.

Wema Sepetu amesema kuwa huu ni mwanzo mzuri na anaahidi kutumia huduma hiyo kutoa elimu kunufaisha jamii,kutangaza sanaa na utamaduni wetu,kuwa karibu na wapenzi ama mashabiki wake wote watakaokuwa wanahitaji kupata habari zake za kweli na uhakika.

Mfumo huo wa kipekee kabisa kwa mwanadada huyo,umezinduliwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye,mfumo ambao utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote."Mfumo wangu huu ni wa kipekee na wa kwanza katika Afrika Mashariki kwa msanii wa tasnia ya Filamu,mfumo huu utaleta fursa nyingi sana zikiwemo ajira kwa vijana na wasanii wenzangu na kutambulika kirahisi"alisema Wema Sepetu.

Kujua mafanikio na Umuhimu wa kazi za Usanii Tanzania,huduma ya Wema Sepetu Mobile ni rahisi na ya uhakika,unatuma neno WEMA kwenda 15404,tayari unakuwa umeishajiunga na utaanza kupokea taarifa na habari za Wema sepetu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno,picha na video kutegemeana na aina ya simu yako unayotumia.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akimpongeza mwanadada Wema Sepetu kwa kubuni mfumo ambao utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote na pia utamsaidia kumuingizia kipato na kuweza kuisaidia jamii inayomzunguka kwa namna moja ama nyingine.
Mtaalamu wa huduma za mitandao kutoka Push Mobile,Haji Yussuph akifafanua jambo kuhusiana na huduma hiyo ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION

Meneja wa Biashara wa Hartmann Trader ambao ndio watoa huduma ya Wema Sepetu Mobile Application,Cecil Mhina akifafanua namna huduma hiyo inavyoweza kutumika na pia maelezo kadhaa namna ya kujinga na kupata taarifa mbalimbali na video kupitia huduma hiyo

Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo adhimu jioni ya leo

Mmoja wa wageni waalikwa akiuliza swali kwa Wema Sepetu namna huduma hiyo inavyoweza kufanya kazi

Wema Sepetu akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na hiyo huduma yake aliyoibuni kwa mashabiki na wapenzi wake itakayobeba mambo mbalimbali kuhusiana na yeye Wema.

Mazungumzo ya hapa na pale yalikuwepo

Waziri Nape akizungumza jambo na Mama Wema Sepetu baada ya uzinduzi kufanyika.

No comments:

Post a Comment