AKIWA
amedumu kwa muda wa siku 360, kocha Stewart Hall wa Azam sasa anahesabu siku
kwa kuwa wiki mbili zijazo atafungasha kilicho chake na kupewa mkono wa kwa
heri ndani ya klabu hiyo.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Azam na
kuthibitishwa na Hall mwenyewe, ni kwamba kocha huyo ameandika barua ya kuachia
ngazi ndani ya klabu hiyo, baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya
Kombe la Shirikisho, huku akivurunda kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Chanzo
hicho kilisema hatua ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuipoka pointi tatu
Azam kwa kumchezesha Erasto Nyoni na hivyo kupoteza matumaini ya ubingwa pia
kimechangia kocha huyo kujichuja.
“Baada ya jana
(juzi) kukatwa pointi na kupoteza matumaini ya ubingwa, kilikaa kikao
cha uongozi na Stewart Hall, moja ya masharti katika mkataba wake ulikuwa ni
kuhakikisha Azam inatwaa ubingwa, na kuchukua Kombe la FA, pia kufanya vizuri
michuano ya kimataifa.
“Kombe
la Shirikisho tumetolewa, ubingwa ndo huo tumeshapoteza dira, ingawa bado tupo
fainali ya Kombe la FA tukitarajiwa kucheza na Yanga, hivyo mwenyewe ameamua
kujiondoa, “ kilisema chanzo hicho.
Kwa
upande wake Hall alipoulizwa jana alikiri kuwepo suala hilo la kuandika barua,
lakini wamekubaliana ataendelea kuinoa timu hiyo hadi ligi itakapomalizika Mei
21 mwaka huu na fainali ya Kombe la FA.
Alisema ameamua kujiondoa kwa sababu amegundua
wachezaji hawamuelewi anachowaelekeza na haoni kama kuna maendeleo kadiri siku
zinavyozidi kwenda.
Sababu
nyingine iliyotajwa na kocha huyo raia wa England, ni pamoja na aina ya
wachezaji waliopo kwenye kikosi chake kutokidhi matakwa yake, huku akidai haoni
mustakabali wa baadaye ndani ya Azam.
Hata
hivyo Katibu Mkuu wa Azam, Nassor Idrissa alipoulizwa jana kuhusu suala hilo
hakuwa tayari kuzungumzia kwa maelezo hakuwa na jipya.
Katika
kipindi alichoiongoza Azam, Hall ameshinda taji moja la Kombe la Kagame Julai
2015, lakini alishindwa kukiongoza kikosi chake kufanya vizuri kwenye mechi za
Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho, ambalo walitolewa
raundi ya pili na Esperance ya Tunisia.
Kocha
huyo raia wa Uingereza, alianza kuinoa timu hiyo Mei 15 mwaka jana akichukua
nafasi ya Mcameroon, Joseph Omong aliyefungashiwa virago, baada ya Azam
kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika na El Merreikh kwa ushindi wa jumla wa
mabao 3-2 na nafasi yake ikachukuliwa kwa muda na aliyekuwa kocha msaidizi,
George ‘Best’ Nsimbe.
Hii
itakuwa ni mara ya pili kwa Hall kutimulia ndani ya klabu, awali alitimuliwa
2014, baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu msimu wa 2013/2014
No comments:
Post a Comment