Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 6, 2016

LIVERPOOL YATINGA FAINALI KUKUTANA NA SEVILLA


MABINGWA Watetezi Sevilla ya Spain wapo njiani kuweka rekodi mpya ya kutwaa UEFA EUROPA LIGI kwa mara 3 mfululizo baada ya kutinga Fainali kwa kuichapa Shakhtar Donetsk 3-1 huko Estadio Ramon Sanchez Pizjuan Jijini Sevilla, Spain.
Timu hizi zilitoka 2-2 katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali Wiki iliyopita huko Nchini Ukraine.
Kwenye mechi hii, Bao za Sevilla zilifungwa na Kevin Gameiro, Bao 2, na Mariano Ferreira Filho.
Sevilla watakutana na Liverpool kwenye Fainali huko Basel, Uswisi hapo Mei 18 baada ya Liverpool kupindua kipigo cha 1-0 cha Mechi ya kwanza na kuiwasha Villareal 3-0 ndani ya Anfield.
Bao za Liverpool zilifungwa na Bruno Soriano, aliejifunga mwenyewe, Daniel Sturridge na Adam Lallana.

Huku wakiwa nyuma 2-0, Villareal walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 70 baada ya Kadi Nyekundu kwa Victor Ruiz kufuatia Kadi za Njano mbili.

Lallana alifunga bao la tatu dakika ya 81na kufanya 3-0 dhidi ya VillarealDaniel Sturridge (Liverpool) dakika ya 63 anaifungia Liverpool bao la pili na mtanange kumalizika dakika 90 kwa 3-1huku Villareal wakiumaliza pungufu 10 uwanjani.Kipindi cha pili dakika ya 71 Víctor Ruiz (Villarreal) alioneshwa kadi ya pili ya njano na kuondoka kwa kadi nyekundu nje

No comments:

Post a Comment