Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 6, 2016

MAROUANE FELLAINI NA ROBERT HUTH WAFUNGIWA MECHI 3 KILA MMOJA

MCHEZAJI wa Manchester United Marouane Fellaini na mwenzake wa Mabingwa wa England Leicester City Robert Huth wamefungiwa Mechi 3 kufuatia tukio la kukwaruzana kwao Jumapili iliyopita kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, BPL, Uwanjani Old Trafford ambayo ilikwisha 1-1.
Kwenye tukio hilo, Huth alimvuta Nywele Fellaini na Kiungo huyo wa Man United kulipiza hapo hapo kwa kumpiga na kiwiko na vitendo hivyo havikuonwa na Refa Michael Oliver na FA, Chama cha Soka England, kiliamua kuwafungulia Mashitaka kwa kuvaana wakati hawana Mpira.
Wachezaji hao Wawili wote walikiri makosa yao lakini Huth aliomba asifungiwe Mechi 3 kwa vile itakuwa Adhabu kubwa kupindukia.
Kifungo hiki kitamfanya Fellaini azikose Mechi 3 za BPL za Man United walizobakiza Msimu huu lakini yupo ruksa kucheza Fainali ya FA CUP hapo Mei 21 Uwanjani Wembley dhidi ya Crystal Palace.

Kwa Huth Msimu wake ndio umekwisha kwa sababu Leicester wamebakiza Mechi 2 tu za BPL ambazo zote atazikosa pamoja na Mechi ya kwanza ya Ligi ya Msimu ujao.
Lakini, Huth yupo ruksa kucheza Mechi ya Fungua Pazia Msimu ujao mpya ya kugombea Ngao ya Jamii ambayo huchezwa Wikiendi moja kabla Msimu mpya wa Ligi kuanza kwa Bingwa wa Ligi, Leicester, kucheza na Bingwa wa FA CUP ambae atakuwa ama Man United au Crystal Palace.

No comments:

Post a Comment